NAIBU Waziri Mkuu Dkt
Doto Biteko, amezindua rasmi Kiwanda cha kuweka Mifumo ya upashwaji Joto Mafuta, itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika kwenye mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP), kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, kilichopo kijiji cha Sojo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho imefanyika leo Machi 26,2024 ambao umeenda sambamba na Utiaji saini Mikataba mitatu, ambayo ni ukodishaji wa eneo la kujenga Miundombinu ya kuhifadhi mafuta (Land Lease Agreement for Marine storage and Terminal Area) Kati ya TPDC na EACOP.
Mradi wa pili ni wa kutumia eneo la Maji (Marine user Rights) kati ya EACOP na Mamlaka ya Bandari Tanga, na Mkataba wa tatu ni wa kufanya shughuli za Bandari (Marine Facility Agreement) Kati ya TPA na EACOP.
Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati, akizungumza wakati wa kuzindua Kiwanda hicho na kushuhudia Utiaji Saini, ameipongeza nchi ya Uganda kwa kushirikiana na Tanzania kuwekeza Mradi huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambalo litachochea uchumi wa nchi zote mbili na kuwaletea maendeleo wananchi.
"Tunaishukuru Serikali ya Uganda kwa ushirikiano huu na nchi ya Tanzania na kuwekeza Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi, ambalo ni kichocheo kikubwa cha uchumi na sisi hatutorudi nyuma tutaendelea kushirikiana kuwekeza kwenye Miradi ya Kimkakati," amesema Biteko.
"Sawa hivi tupo kwenye Majadiliano kuwekeza kwenye Gesi Asilia na Nchi ya Uganda"ameongeza Biteko.
Aidha,amewataka Watanzania kuendelea kuzipatia ushirikiano Sekta binafsi katika Uwekezaji, pamoja na kuacha kuwa na Migogoro ya ardhi ili waendelee kuwekeza na kukuza uchumi na kuwaletea Maendeleo.
Pia amewataka Watanzania hasa wale ambao wanapitiwa na Mradi huo wa Bomba la Mafuta,kwamba wawe walinzi wa mradi huo pamoja na kutunza miundombinu yake.
Katika hatua nyingine amewaonya Watanzania kutotumika na Makampuni ya Nje na kufanya udanganyifu ili wapate kazi kwenye Miradi ya Kimkakati (Local Content) na kuwanyima fursa wenzao na kwamba Kampuni hizo zote zitafutwa.
Amewataka pia Wakandarasi Wazawa pamoja na Watanzania ambao wamepata kazi kwenye Miradi ya Kimkakati, kwamba wafanye kazi zako kwa Uaminifu na ili kujenga sifa ya Watanzania na kuendelea kupata kazi zaidi.
Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini nchini Uganda Ruth Nankwabira, amesema uwekezaji huo wa Bomba la Mafuta, unaimarisha miundombinu ya Nishati,na kwamba mpango huo unasisitiza dhamira ya kuimarisha usalama wa Nishati na kukuza ushirikiano wa nchi hizo mbili, na kusema kwamba undugu na ushirikiano uendelee kwa Tanzania na Uganda.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo Petrol Tanzania (TPDC)Mussa Makame, amesema Mradi huo wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda lina urefu wa Kilomita 1,443 na kwamba wamewekeza Hisa Sh.bilioni 820 na hadi sasa wameshatoa Sh.bilioni 710.
Amesema kwa upande wa Fidia wameshalipa wananchi asilimia 99.2 ambapo nyumba 340 zimeshajengwa na Mradi huo ujenzi wa Bomba la Mafuta upo asilimia 27.
Mbunge wa Jimbo la Bukene Selema Zedi, amesema Mradi huo wa Bomba la Mafuta umekuwa na Manufaa Makubwa ambapo wananchi wamepata Ajira, kujengewa nyumba pamoja na kupewa Chakula na kulimiwa na hata kujengewa miundombinu ya Barabara.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha, ametoa wito kwa wananchi kwamba waendelee kuchungulia fursa za ajira kwenye mradi huo ili wajipatie vipato na kuinuka kiuchumi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Stephen Byabato,umetumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Mseven kwa uwekezaji huo Mkubwa wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki EACOP na kuunganisha Mstari kutoka Hoima Uganda Hadi Chongoleani Tanga.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Stephen Byabato akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo Petrol Tanzania (TPDC)Mussa Makame,akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika wa EACOP Martin Tiffer akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Mbunge wa Jimbo la Bukene Seleman Zedi akizungumza kwenye Uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini Nchini Uganda Ruth Nankwabira akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati akizindua Kiwanda hicho.
Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati akishuhudia Utiaji Saini.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Uzinduzi wa Kiwanda hicho ukiendelea.
Uzinduzi wa Kiwanda hicho ukiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Social Plugin