Na Mariam Kagenda _ MULEBA
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema hayo leo hii wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa tayari ugonjwa huo umeishaenea katika Wilaya hiyo hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.
Dkt. Nyamahanga amesema kuwa pia wamepiga marufuku uuzaji wa matunda yaliyomenywa kwa kipindi hiki huku wakitakiwa kushiriki kufanya usafi kikamilifu ili kujikinga na ugonjwa huo wa kipindupindu katika Wilaya ya Muleba.
Aidha amesema kuwa dalili za ugonjwa wa kipindupindu ni kutapika, kuhara pamoja na mwili kuishiwa nguvu hivyo endapo mtu akihisi kuwa na dalili za ugonjwa huo anatakiwa kufika kwenye kituo cha afya ili aweze kupata matibabu haraka.
Kwa upande wake Afisa Afya Wilaya ya Muleba Bw. Johanes Mtoka amesema kuwa tangu ugonjwa huo ulipotiwe tarehe 14 Desemba 2023 jumla ya watu sita wamefariki huku wagonjwa wakiwa 146 ambapo wametibiwa na kuruhusiwa .
Social Plugin