Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RC MNDEME AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SHINYANGA..AANIKA VIPAUMBELE KUINUA WANAWAKE, ATAHADHARISHA UKIMWI


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaongoza wanawake katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga ambapo ametumia fursa hiyo kuwasihi wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi zijazo huku akiwakumbusha kujihadhari na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwani kwa mkoa huo bado hali si shwari.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Mkoa wa Shinyanga yakiongozwana kauli mbiu ‘Wekeza kwa Wanawake ; Kuharakisha Maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii’ yamefanyika leo Ijumaa Machi 8,2024 katika viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na makundi mbalimbali ya wanawake.


Amesema kutokana na tafiti ya kisayansi iliyofanyika mwaka 2022 (THIS 2022), mkoa wa Shinyanga una ushamiri wa maambukizi ya VVU ya asilimia 5.6 ambayo ipo juu ya kiwango cha taifa cha asilimia 4.5.

“Serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea kuratibu udhibiti wa maambukizi ya VVU kwa kutoa huduma mbalimbali za tiba na matunzo. Pamoja na jitihada zote zinazofanyika za kuwawezesha wanawake, nawakumbusha kujilinda dhidi ya maambukizi ya VVU kwani hupelekea kupunguza nguvu kazi, kuongezeka kwa yatima, wajane na hatimaye kusababisha jamii kuzama kwenye wimbi la umaskini”,amesema Mhe. Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewakumbusha kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kufuata maelekezo ya watalaam wa afya na kuhakikisha usafi wa mazingira katika maeneo yanayowazunguka.

Katika hatua nyingine amewataka Wanawake mkoani Shinyanga wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha Mpito ambapo Serikali inaendelea kufanya maboresho juu ya utoaji wa mikopo asilimia 10 katika Halmashauri huku akiwatahadharisha wanawake wajiepushe na mikopo kausha damu ambayo inawarudisha nyuma kiuchumi.

Amesema serikali imeendelea na jitihada za kuwezesha wanawake kiuchumi ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi mbalimbali za kifedha.

“Mkoa wa Shinyanga unaungana na nchi zingine duniani kuratibu na kusimamia uwekezaji katika kundi la wanawake kwa kuweka vipaumbele katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wanawake, kuendeleza jitihada za serikali na wadau wa maendeleo za kupinga mila na desturi zenye madhara zinazopelekea kukosekana kwa usawa kijamii, kiuchumi na kisiasa”,amesema Mhe. Mndeme.


Amesema pia Mkoa wa Shinyanga unaendelea kuboresha na kusimamia utoaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto katika vituo vya kutolea huduma na kusimamia chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi inayotolewa kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 14.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa nne kushoto) akicheza na wanawake wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

“Tunaendelea kuboresha mazingira ya elimu kwa kuhakikisha mkoa unakuwa na shule bora za wasichana, kuhamasisha matumizi ya teknolojia rahisi kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali ili kuongeza ubora wa bidhaa wanazotengeneza zikiwemo batiki, sabuni, mafuta, viungo vya chakula n.k”,amesema.

“Kipaumbele kingine ni kusimamia programu Jumuishi ya taifa ya malezi na makuzi na maendeleo ya watoto kuanzia miaka 0 hadi 8 na kuendelea kuratibu na kusimamia uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kupitia baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, mfuko wa wanawake na kupitia kwa wadau mbalimbali walio ndani na nje ya mkoa”,ameongeza Mhe. Mndeme.

Hali kadhalika Mkuu wa Mkoa, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaamini wanawake na kuwapatia fursa mbalimbali za uongozi, na wamewakuwa wakifanya vizuri kwa kuiga uongozi wake na kuwatumikia wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Mhe. Mndeme amewashukuru wadau mbalimbali waliotoa michango yao kufanikisha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri, Idara ya maendeleo ya jamiiTANROADS, Shirika la YAWE, Life Water International, Rafiki SDO, TCRS, ADD international na ICS.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi mkoa wa Shinyanga Dkt. Regina Malimi ambaye ni katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Taifa amesema miongoni mwa changamoto zinazowakwamisha wanawake ni mikopo umiza hivyo kuwataka wanawake kuacha kujiingiza kwenye mikopo hiyo.

 Aidha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuasisi Jukwaa hilo ambalo limekuwa chachu ya kuwainua wanawake kiuchumi huku akiiomba Serikali kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wanawake, likiwamo tatizo la mikopo kausha damu, mila na desturi kandamizi pamoja na vitendo vya ukatili.

Kwa upande wao, Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga akiwemo Mhe. Santiel Kirumba, Dkt. Christina Mzava na Lucy Mayenga na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi wamewataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto pamoja na kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utaofanyika mwaka huu.

"Tunampongeza sana Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kuendelea  kuwaamini wanawake na kuwapatia nafasi mbalimbali za uongozi, na wamekuwa wakifanya vizuri kwenye utendaji wao kazi",ameongeza Mhe. Kirumba.

Katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau wa maendeleo ikiwemo chakula kwa ajili ya watoto ambao ni Wahanga wa Ukatili katika Kituo cha Agape na mifuko 31 ya saruji kwa ajili ya ujenzi Bweni katika shule ya Buhangija iliyotolewa na Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Shinyanga (TPF- NET Mkoa wa Shinyanga).

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku Ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi mkoa wa Shinyanga Dkt. Regina Malimi ambaye ni katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Taifa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa TPF-NET Mkoa wa Shinyanga akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme mifuko 31 ya saruji kwa ajili ya ujenzi Bweni katika shule ya Buhangija iliyotolewa na Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Shinyanga (TPF- NET Mkoa wa Shinyanga)
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikabidhi chakula kilichotolewa na wadau kwa ajili ya watoto ambao ni Wahanga wa Ukatili katika Kituo cha Agape.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kushoto) akicheza na wanawakewakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga






Awali Wanawake wakiwa katika Maandamano.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea
Maandamano yakiendelea.

Picha na Marco Maduhu na Kadama Malunde
@malundeblog

Shangwe Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga.... Wanawake wakicheza live

♬ original sound - Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com