Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WOMEN FOR CHANGE WATOA MSAADA WA SOFA NA VITI MWENDO KWA WAZEE NA WASIOJIWEZA KOLANDOTO

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC), kinachojihusisha na Ununuzi wa Hisa ili kuinuana kiuchumi na chenye mfuko wa kusaidia jamii na watoto walioko kwenye mazingira magumu kimetoa msaada wa Sofa nne zenye kukaliwa na watu nane na Viti Mwendo (Wheel Chairs) viwili vyenye thamani ya Shilingi Milioni 1.6 kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mjini Shinyanga.

Kikundi cha Women For Change kimetoa msaada huo leo Jumatano Machi 13,2024 kuelekea kwenye Kongamano Maalumu la wanawake wa Shinyanga maarufu 'Shy Women’s Day Out linaloendeshwa na Women For Change ambalo linatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi Machi 16,2024 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi sofa na viti Mwendo, Mwenyekiti wa Kikundi cha Women For Change bi. Ansila Benedict amesema kikundi hicho chenye wanachama 20 kimetoa msaada huo ikiwa ni utamaduni wao wa kusaidia makundi yenye uhitaji mbalimbali katika jamii.

“Tumeona leo tuje kuwatembelea wazee wetu wa Kolandoto, huwa tunafanya hivyo kwa watu mbalimbali wenye uhitaji wakiwemo wazee, watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Katika kuangalia makundi yenye uhitaji tumeamua kuja hapa Kolandoto baada ya kuelezwa mahitaji yanayotakiwa",amesema Ansila.
Wanachama wa Women For Change wakikabidhi sofa na Viti Mwendo kwa Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mjini Shinyanga.

"Tumekuja tu kutatua baadhi ya changamoto na Mungu akitujaalia kwa wakati mwingine tuweze kutatua na nyinginezo ikiwemo chakula. Leo sisi Women For Change tumeleta Sofa nne (Set nne) za kukaliwa na watu nane na viti mwendo (Wheel Chairs) viwili vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.6", ameongeza Ansila.

Kwa upande wake, Afisa ustawi wa jamii Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Sophia Kang'ombe amesema hivi sasa makazi hayo sasa ya jumla ya wahitaji 18 kati yao wanaume ni 11 na wanawake saba ambapo ametumia. fursa hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kufika katika makazi hayo ya wazee na kutatua changamoto zilizo.

Diwani wa kata ya Kolandoto, Mussa Andrew amewapongeza wanachama wa kikundi cha Women For Change kwa kuwakumbuka na kuwathamini wazee hivyo kuwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kusaidia wazee hao kwani mahitaji ni mengi ikiwemo chakula na nguo.

Nao baadhi ya wazee akiwemo Catarina Maige na Kija Jipuge wamewashukuru wanachama wa Women For Change kwa kufika katika makazi ya wazee na kuwapatia misaada mbalimbali na kuwaomba wasichoke kufika kuwaona na kuwapatia mahitaji mbalimbali.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women For Change bi. Ansila Benedict akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo (Wheel Chairs) viwili vyenye thamani ya Shilingi Milioni 1.6 kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women For Change bi. Ansila Benedict akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mjini Shinyanga.

Afisa ustawi wa jamii Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Sophia Kang'ombe akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Wanachama wa kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) wakikabidhi sofa na Viti Mwendo (Wheel Chairs) kwa wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mjini Shinyanga.

Wanachama wa kikundi cha Wanawake na Mabadiliko Manispaa ya Shinyanga (Women For Change - WFC) wapiga picha ya pamoja na wazee wakati wakikabidhi sofa na Viti Mwendo kwa wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mjini Shinyanga.
Mhasibu wa Kikundi cha Women For Change bi. Faustina Kivambe akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Women For Change wakiwa katika makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto
Wanachama wa kikundi cha Women For Change wakiwa katika makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto
Wanachama wa kikundi cha Women For Change wakiwa na wazee katika makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto
Wanachama wa kikundi cha Women For Change wakiwa na wazee katika makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto
Mwanachama wa Kikundi cha Women For Change bi. Anascholastica Ndagiwe (MC Mama Sabuni) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo
Mwanachama wa Kikundi cha Women For Change bi. Anascholastica Ndagiwe (MC Mama Sabuni) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo
Diwani wa kata ya Kolandoto, Mussa Andrew akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo
Bi. Catarina Maige akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo
Mzee Kija Jipuge akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wa Sofa nne na Viti Mwendo
Wazee wakicheza muziki
Wanachama wa kikundi cha Women For Change na viongozi mbalimbali wakipiga picha ya kumbukumbu katika makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto
Wanachama wa kikundi cha Women For Change wakipiga picha ya kumbukumbu katika makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com