Afisa elimu wa mkoa wa Pwani Bi. Sarah Mlaki akihutubia hadhira ya jumuiya ya shule ya msingi Kibiki. Kutoka kushoto Kamishna wa skauti Wilaya ya Kibaha Bi. Azama Hassan, Afisa elimu ya watu wazima halmashauri y a Chalinze , Selemani Nkunguu, Kamishna wa mkoa wa Pwani Bi. Safi Shabani na Afisa mazingira wa halmashauri ya Chalinze Bi. Blandina Mgimba
***
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
AFISA elimu wa Mkoa wa Pwani Mwalimu Sarah Mlaki amekemea vikali vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa dhidi ya wanafunzi na watoto kwa ujumla.
Kauli hiyo ameitoa alipokuwa kwenye zoezi la upandaji miti lililoratibiwa na Jumuiya ya skauti halmashauri ya Chalinze chini ya Kamishna wake Mwalimu Ester Kalale, kwenye viwanja vya shule ya msingi Kibiki leo.
Mwalimu Mlaki amesema watu waovu hawana nafasi ya kutamba katika jamii.Wachukuliwe hatua kali. Na kuwaasa wanafunzi watoe taarifa zozote za ukatili kwa wazazi, walimu na hata kutumia masanduku ya maoni.
Mwalimu Mlaki pia amewapongeza walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kibiki kwa kuboresha mazingira ya kitaaluma ikiwa pamoja na mikakati ya ujanishaji shuleni hapo.
Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundo mbinu ya shule nchini pamoja na kuinua kiwango cha taaluma kwa kuwezesha walimu kupata mbinu mpya ya mafunzo ya kiingereza na sayansi nchini.
Zoezi hilo la uzinduzi wa kitalu cha miti shuleni hapo lilihudhuriwa pia na Kamishna wa skauti Mkoa wa Pwani Bi. Safi Shabani, Kashna wa Wilaya ya Kibaha Bi. Azama Hassan, Afisa mazingira wa halmashauri ya Chalinze Bi. Blandina Mgimba, baadhi ya Wanafunzi wa Skauti halmashauri ya Chalinze Pamoja jumuiya ya shule ya msingi Kibiki.
Social Plugin