Na Mariam Kagenda _ Kagera
Basi la Shule ya Sekondari Kemebos lenye namba za usajili T 770 DSQ limepata ajali na kuua mwanafunzi mmoja na kujeruhi wengine sita katika Kata ya Kimwani Wilayani Muleba Mkoani Kagera wakati likisafirisha wanafunzi kutoka Bukoba kuelekea Mkoani Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema kuwa ajari hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane za usiku Kata ya Kimwani Wilayani Muleba ambalo lilikuwa na jumla ya wanafunzi 35.
Dkt. Nyamahanga amesema kuwa Mwanafunzi huyo ni wa kidato cha tano aliyejulikana kwa jina la Frank Matage mwenye umri wa miaka 17 wa shule ya Sekondari Kemibos iliyoko manispaa ya Bukoba huku majeruhi hao sita wote wamelazwa katika Hospital ya rufaa ya Mkoa Bukoba .
Aidha Dkt. Nyamanga amesema kuwa kwa taarifa za awali zinaeleza chanzo cha ajali hiyo ni Mwendo kasi wa Dereva ambaye alishindwa kukata kona.
Social Plugin