Mwakilishi wa Msimamizi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP, Bw. Guillaume Mallevaey (kulia) akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Hesabu za Serikali (PAC) imepongeza kasi ya ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania likiwa na urefu wa kilomita 1443.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga, wametembelea na kujionea utekelezaji wa mradi huo leo Jumanne Machi 19,2024 katika Kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Japhet Hasunga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa uwekezaji mkubwa kwa kushirikiana na serikali ya Uganda na Ufaransa kwa kuwekeza katika mradi huo ambao unatengeneza ajira hivyo kupunguza umaskini.
Mhe. Hasunga amesema malengo ya Kamati kutembelea mradi huo ni kuona fedha za umma zilizoidhinishwa na Bunge zimetekelezwa ipasavyo na kuendana na thamani ya mradi (value for Money) na kwamba mara baada ya kutembelea kiwanda cha hicho Wajumbe wa Kamati wameridhika na maendeleo ya ujenzi huo.
"Tumekuja hapa kuangalia fedha zilipitishwa na Bunge zimetumikaje na zinaendelea kutumikaje pia tumekuja kujifunza kiwanda hiki kinajengwaje na je kitatoa mchango gani katika taifa letu. Na sisi Kamati tumeshuhudia kiwanda hiki ni muhimu sana na kitatoa mchango mkubwa katika taifa letu kwa kuhakikisha uchumi wetu unakua, hiki ni kiwanda hicho tutakuwa tunaketeleza sera yetu ya viwanda. Pia faida ya ajira kwa vijana wetu, na tutapunguza umaskini kwa vijana na jamii inayozunguka inanufaika na mambo mbalimbali",amesema Mhe. Hasunga.
"Tumekuja kuangalia je uwekezaji huu una tija kiasi gani na utaisaidiaje nchi katika kukabiliana na suala la umaskini. Kwa hiyo hili tumeliona na tumeridhika na kazi inayoendelea hapa, mradi unaendelea vizuri ,fedha zinatumika vizuri. Tumeona kazi kubwa inayofanywa na EACOP, tumeshuhudia uwekezaji mkubwa uliofanyika, tumeona tayari mabomba yamefika kwa kweli manufaa makubwa yanaonekana ikiwemo suala la fidia kwa wananchi na kujengewa nyumba",ameongeza Mhe. Hasunga.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mussa Makame, amesema mpaka sasa ujenzi wa kiwanda hicho umefikia asilimia 61, mabomba yameshaanza kuwasili na wanatarajiwa ifikapo mwezi Aprili 2024 kiwanda kitaanza kufanya kazi na Machi 26,2024 Mhe. Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kufungua rasmi kiwanda hicho.
Mwakilishi wa Msimamizi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP, Bw. Guillaume Mallevaey amesema mradi huu uko vizuri na Shughuli zote walizozianisha wameanza kuzitekeleza na mitambo imejengwa tayari na mabomba yamewasili kwa wingi.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Naitwapaki Tukai amesema utekelezaji wa mradi unaendelea vizuri vizuri na kumekuwepo na ushirikishwaji mzuri wa jamii inayozunguka mradi ili kuhakikisha wanafaidika na mradi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza leo Jumanne Machi 19,2024 wakati Wajumbe wa kamati hiyo walipofika katika Kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora kutembelea Mradi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Picha na Kadama Malunde 1 blog
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza wakati Wajumbe wa kamati hiyo walipofika katika Mradi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mussa Makame akizungumza wakati Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali walipofika katika Mradi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Naitwapaki Tukai akizungumza wakati Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali walipofika katika Mradi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakiwa katika Mradi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP
Mwakilishi wa Msimamizi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP, Bw. Guillaume Mallevaey akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho.

Mwakilishi wa Msimamizi wa ujenzi wa kiwanda kitakachokuwa kikiweka mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba yatakayotumika katika mradi wa EACOP, Bw. Guillaume Mallevaey (katikati) akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog