Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA CHASHAURI MAREJEO YA SHERIA YA KIKOKOTOO




Na Dotto Kwilasa, DODOMA 


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinashauri Bunge kufanya marejeo ya sheria ya kikokotoo ambayo yatawezesha kufanyika kwa maboresho ambayo yataleta ahuweni kwa watanzania wa hali ya chini.

Aidha kimepinga kitendo cha Bunge kupitisha sheria ya wenza wa viongozi kulipwa mafao huku kikishauri kufanyiwa kwa marejeo ya sheria ya Kikokotoo ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na watumishi.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Catherine  Ruge, alibainisha hayo jana jijini hapa, alipokuwa akitoa hutuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Amesema inasikitisha kuona Wabunge ambao wamechaguliwa na wananchi kwenda kuwatetea wananchi wanao kabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo umasking wanakuwa time ya kusifu na kuabudu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Freeman Mbowe, amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu 2025 utakuwa wa kufa na kupona kwakuwa wataweka wagombe kila nafasi itakayo tangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Amesema kwa kufanya hivyo hakuna mgombe yeyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye atapita bila kupigwa kama ambavyo imekuwa katika miaka iliyopita.

Mbowe, amesema katika uchaguzi huo CHADEMA wamepanga kuwe mgombe kila nafasi itakayo tangazwa na NEC, katika ngazi zote kuanzia kitongoji hadi taifa.

"Lazima mhakikishe kila eneo anapatikana mtu wa kwenda kugombea na awe na uwezo wa kushinda siyo kushiriki na kwa kiongozi yoyote ambaye atashindwa kuweka mgombea chama hatutamchekea katika hilo tutachekea kwa mambo mengine siyo hilo lazima tuwe na uchungu sisi ndiyo tutaweza kuondoa huu msiba wa CCM"anasisitiza Mbowe

Alisema CHADEMA ndiyo Chama pekee ambacho kitakwenda kumaliza malalamiko ya wananchi ambak hivi sasa wanalalamikia ugumu wa maisha.

Aidha, alisema wanachoomba ni Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya kwani ndiyo itasaidia kumaliza tabia ya kuingia madarakani kwa viongozi ambao hawana kibali cha watu na Mungu.

"Asilimia 90 ya viongozi waliopo madarakani hivi sasa wengi wao wamengia katika nafasi hizo kwa njia zisizo za haki kutokana na uwepo wa tume hii ya uchaguzi hali ambayo imesababisha uwepo wa ufisadi,uminyaji haki na uvunjifu wa demokrasia nchini"alisema

Alisema hivi sasa wanachi wanalalamika gharama za maisha kupanda lakini wabunge ambao wamechaguliwa kuwawakilisha wananchi wanajiongozea mishahara.

"Mfumuko wa bei umepanda mara tatu lakini wabunge mwaka jana wamejipandishia mishahara hadi milioni 18 kwa mwezi"alisema Mbowe

Mwenyeki wa BAWACHA Taifa Sharifa Sulaiman, alisema wanawake wengi wameonyesha nia ya kugombe nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao ikiwemo nafasi ya Urais.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com