Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiambatana na Viongozi wa Chama na Serikali ngazi ya taifa na Mkoa wa Mwanza, ametembelea Familia ya Mzee Pastory Makungu (RPC Mstaafu) na Bi. Ellen Bogohe, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, eneo la Iseni, Magu, mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuhani na kuwapatia pole kufuatia msiba wa mwanafamilia yao, Bi. Queen Elizabeth Joseph Ngayilijiwa (Bogohe) aliyefariki Jumatatu Machi 25, 2024 na kuzikwa Machi 27, 2024.
Mbali ya kuhani msiba huo, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi pia alipata wasaa kwenda kumsalimia Bi. Ruth Kabula Bogohe, mstaafu mwenye miaka 88, ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa NEC ya CCM Taifa kwa miaka 15, Mwenyekiti wa UWT kwa miaka 10 na Katibu Tarafa maeneo mbalimbali nchini kwa miaka 25.
Viongozi wengine waliombatana na Balozi Dk. Nchimbi, ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Komredi Michael Lushinge (Smart), Mjumbe wa NEC Taifa, Komredi Richard Kasesera, Katibu wa Mkoa wa Mwanza, Komredi Omari Mtua, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Mwanza, Komredi Jamal Babu na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ndugu Amina Makilagi (kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza).
Social Plugin