Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DK. NCHIMBI AWASILI ZIMBABWE MKUTANO WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akisalimiana na kuzungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Mama Sophia Shaningwa walipokutana mara baada ya kuwasili nchini Zimbabwe, leo mchana Machi 17, 2024, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, utakaofanyika nchini humo.

************


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiambatana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya CCM ya Taifa (NEC), amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), ambao pamoja na masuala mengine utajadili maendeleo ya mshikamano wao na kuuendelea kuuimarisha zaidi.

Mkutano huo ambao pia utashirikisha watendaji wakuu wa Jumuiya za Wazazi, Wanawake na Vijana wa vyama hivyo, utafanyika kwa siku tatu, kuanzia Machi 17 hadi 20, 2024, katika Mji wa Victoria Falls, kwa ajili ya kujadili agenda mbalimbali zinazohusu urafiki na uhusiano wa vyama hivyo ambavyo vyote viko madarakani, vikiongoza Serikali na Nchi husika.

Katika msafara wake, Katibu Mkuu Balozi Dk. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Komredi Gilbert Kalima, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM), Komredi Fack Raphael Lulandala, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Zanzibar, Komredi Tunu Juma Kondo.

Mbali ya Chama Cha Mapinduzi, vyama vingine vinavyoshiriki mkutano huo ni pamoja na mwenyeji ZANU – PF (Zimbabwe), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), ANC (Afrika Kusini) na Botswana Democratic Party (BDP – cha Botswana).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com