Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiongoza Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan, Jumamosi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, walipokutana Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Abeid Amani Karume. Dk. Nchimbi amewasili Zanzibar leo Jumamosi, Machi 2, 2024, akitokea nchini India, ambako amelazimika kukatisha ziara yake ya kikazi, kushiriki msiba wa Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akimpatia pole Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi (Mb), ambaye ni mmoja wa watoto wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Mwinyi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akimpatia pole Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dk. Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni mmoja wa watoto wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili Hayati Mwinyi, Machi 2, 2024, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akimpatia pole mmoja wa Wajane wa Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Bi Siti Mwinyi (aliyekaa), baada ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Mwinyi, shughuli iliyofanyika Jumamosi, Machi 2, 2024, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Social Plugin