Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Haruna Lipumba (wa pili kutoka kulia pichani) na Mwenyekiti wa Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), Ndugu Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam, Ndugu Abbas Mtemvu, baada ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Jumanne, Machi 12, 2024, Ikulu, Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na mmoja wa wasanii nyota na maarufu wa Mziki wa Bongofleva, Ndugu Rajab Abdul Kahali 'a.k.a' Harmonize, kutoka Kundi la Muziki la Konde Music Worldwide, walipokutana baada ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Jumanne Machi 12, 2024, Ikulu, Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akizungumza jambo na Viongozi wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Simba, ambao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdalla Muhene (aliyeshikana nae mkono), Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu (kushoto kwa Dk. Nchimbi) na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Ahmed Ally (wa pili kutoka kulia pichani), huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam, Ndugu Abbas Mtemvu (wa tatu kutoka kulia pichani), Katibu wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam, Ndugu Adam Ngalawa (wa kwanza kulia) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Ndugu Juma Simba ‘Gadafi’ wakifuatilia mazungumzo hayo. Ilikuwa wakati wa futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Komredi Abdulrahman Kinana, akisalimiana na kuzungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, walipokutana kwenye futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, jioni ya leo Jumanne Machi 12, 2024, Ikulu, jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam, Ndugu Abbas Mtemvu (katikati), Katibu wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam, Ndugu Adam Ngalawa (kulia), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Juma Simba ‘Gadafi’ (mwenye kanzu ya kijani) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Ndugu Toba Nguvila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar Es Salaam (kushoto).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa, Qaillah Bilal (mwishoni kushoto), baada ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, leo Jumanne, Machi 12, 2024, Ikulu, Dar Es Salaam. Wengine pichani ni pamoja na Nurdin Bilal ‘Shetta’, (mwishoni kulia) ambaye ni mzazi wa Qaillah.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na kufurahia jambo na Ndugu Juma Simba ‘Gadafi’, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (mwenye kanzu ya kijani), Ndugu Toba Nguvila, Katibu Tawala (RAS) wa Mkoa wa Dar Es Salaam (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media Group Ndugu Nasib Abdul Isack (Diamond platinumz), ambaye pia ni mmoja wa wasanii nyota na maarufu wa Mziki wa Bongo Fleva na mfanyabiashara, alipokutana nao kwenye futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, leo Jumanne, Machi 12, 2024, Ikulu, Dar Es Salaam.
Social Plugin