Na Ferdinand Shayo ,Manyara
Leo Machi 12 mwaka 2024 ni Siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Bilionea David Mulokozi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited ambapo Keki yake imekatwa na Watoto yatima wa kituo cha Hossana Homecare Foundation ambapo Watoto hao wamepatiwa misaada mbali mbali ikiwemo vyakula na vifaa vya usafi ,misaada yote ikiwa na thamani ya shilingi milioni 10.
Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba yake Meneja Rasilimali Watu wa kampuni ya Mati Super Brands Doreen Raphael amesema kuwa licha ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo kuwa nje ya mkoa wa Manyara Kikazi lakini wameamua kukata keki hiyo na kuwapatia Watoto yatima Pamoja na kutoa misaada mbali mbali ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka.
Mkurugenzi wa Kituo hicho Neema Munisi ameipongeza Kampuni hiyo kwa kutoa misaada mbali mbali kila mwaka ambayo imekua ikiwasaidia Watoto yatima wanaolelewa katika kituo hicho.
Social Plugin