Na Dotto Kwilasa,DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwaongoza viongozi mbalimbali kwenye ibada maalum ya kumbukizi ya miaka 40 ya Hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania katika kipindi cha awamu ya Kwanza.
Ibada hiyo itakayofanyika siku ya Ijumaa Aprili 12, 2024, saa 3:00 asubuhi, imeandaliwa na familia ikishirikiana na Taasisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine.
Hayo yameelezwa leo Marchi 28,2024 jijini hapa na Msemaji wa Familia hiyo Lembris Marangushi Kipuyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amemtaja Hayati Sokoine kuwa alikuwa mzalendo wa kweli, aliyependa taifa lake na wananchi wake kwa kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika na watanzania wote.
"Tunafahamu Hayati Sokoine aliwatumikia wananchi bila kubagua na alikuwa na hofu ya Mungu katika kufanya kazi zakezake, Sokoine Alizaliwa Agosti 01, 1934, kijijini Enguik, Monduli Juu wilayani Monduli, mkoani Arusha, " amesema
Hayati Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika vipindi viwili wakati wa uongozi wa Awamu ya Kwanza, Rais akiwa Hayati Julius Kambarage Nyerere ambapo alizaliwa Agosti 01, 1934, kijijini Enguik, Monduli Juu wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Aidha aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari, 1977 hadi 7 Novemba, 1980 na mara ya pili kuanzia tarehe 24 Februari, 1983 hadi tarehe 12 Aprili, 1984 alipofariki kutokana na ajali ya gari. Huko eneo la Wami Dakawa mkoani Morogoro akitokea Dodoma kwenye kikao