Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Mfuko wa SELF Bw. Petro Mataba akiwasilisha mada katika kikao hicho.
Bw. Sabato Kosuri Afisa Mawasiliano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina akifafanua jambo wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika jengo la Mafao House Ilala jijini Dar es Salaam.
Mfuko wa SELF MICROFINANCE FUND umeongeza upatikanaji wa huduma za mikopo kwa wananchi wenye kipato cha chini na kati ambapo Desemba 12, 2023 Mfuko ulitoa mikopo ya bilioni 324.
Hayo yamesemwa leo Machi 11, 2024 na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Mfuko wa SELF Bw. Petro Mataba wakati akizungumza katika kikao kazi kati ya jukwaa la Wahariri Tanzani (TEF) kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika Jengo la Mafao House Ilala Jijini Dar es salaam.
Amesema mikopo iliyotolewa iliwafikia wanufaika laki 3 na elfu 14 ambapo kati yao wanawake ni laki 166,000 wanaume laki 147,000 ambao walitoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Amesema Mfuko wa SELF unafanya kazi nchi nzima kupitia matawi 12 na hadi sasa wanazaidi ya taasisi 200 ambazo wanazikopesha,pia Mfuko huo umetengeneza ajira elfu 37 kutokana na wanufaika wanaochukua mikopo sanjari na kutoa elimu ya fedha kwa wanufaika 1517.
Akielezea majukumu ya mfuko huo Bw.Mataba amesema ni kutoa huduma za mikopo midogo kwa watu binafsi,vikundi na taasisi ndogo za fedha zinazolengwa na Serikali ili kukuza sekta ya huduma ndogo za fedha kwa ajili ya kupunguza umasikini.
Pia wanatambua,kuendeleza na kukuza fursa za kuwawezesha ajira wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo,elimu ya utendaji kazi na mafunzo kwa ajili ya kuboresha stadi zao.
Aidha, ameeleza kuwa wanaandaa na kuweka utaratibu na mikakati ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili kuwawezesha kupata huduma za kifedha kwa ajili ya kujiajiri kwa tija.
“Tunamikopo ya taasisi ndogo za kifedha na riba inayotolewa kwa mikopo hii ni kati ya asilimia 16 na 18 ili waende kuwakopesha wanufaika wa biashara na kilimo”, amesema
Social Plugin