Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka inadaiwa amenusurika Kifo baada ya Gari lake kushambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.
Taarifa mbalimbali zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaeleza tukio hilo limetokea eneo la Ndaleta, wilayani Kiteto wakati Ole Sendeka akiwa na dereva wake akielekea jimboni kwake Simanjiro.
Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kupitia Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mwakatundu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo amesema limetokea majira ya jioni leo Ijumaa Machi 29, 2024 na washambuliaji wakitokomea.
Endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi.
Social Plugin