Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA WAGHARAMIA MATIBABU YA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

 


Na Dotto Kwilasa, Dodoma

OFISI ya Taifa ya Mashtaka imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa waliolazwa kwa muda mrefu kwenye hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni hatua ya kuenzi siku ya wanawake Duniani Machi 8 mwaka huu. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kukabidhi fedha na vitu mbalimbali kwa wagonjwa, Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Chivanenda Luwingo, amesema msada huo ni sehemu ya matendo ya huruma wakati huu wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

"Kuelekea siku hii ya wanawake Duniani sisi wanawake wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tulikuja hapa kuona changamoto zilizipo kwa wagonjwa hivyo tukabaini uwepo wa wagonjwa wa muda mrefu ambao gharama za matibu kwao zimekuwa kubwa.

"Hivyo leo hii tutawalipoa gharama matibabu wagonjwa hawa wa muda mrefu watano pamoja na mtoto mmoja ambaye anahitaji gharama za upasuaji na dawa kwa muda wa siku saba jumla ya gharama za matibabu yote ni 900,000"alisema

Pia, alisema pamoja kugharamia matibabu hayo pia wametoa vitu mbalimbali kwa manusura wa ukatili wa kijinsi ikiwemo watoto waliyupwa wa wazazi wao.

"Tumetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto manuscript wa ukatili ambao waliputwa na wazai wao hvyo wanahitaji vitu kama nepi, maziwa pamoja na dawa mbalimbali lakini pia tumetoa msaada wa sabuni na mafuta jumla gharama zote.inakuwa ni Sh. milioni mbili"amesema

Muuguzi Mfawidhi wa hospitali ya rufaani mkoa wa Dodoma Stanley Mahundo, aliishukuru Ofisi ya Taifa ya Mashtak kwa msaada huo ambao utakwenda kusaidia wagonjwa wenye uhitaji.

"Tunaishukuru sana Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa msaada huu na tunaahidi kuwa tutahakikisha msaada huu unawafikia walengwa na nitoe wito kwa watu wengine kujitoa kusaidia wagonjwa kama hawa"amesema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com