Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jason Rweikiza ametoa Sadaka ya FUTARI kwenye Misikiti 113 iliyopo jimboni kwake.
Katibu wa Mbunge,Mhe Jason Lwankomezi amesema kuwa Futari hiyo itawafikia waamini wa Dini ya Kiislaam kupitia Misikiti iliyopo katika maeneo yao.
Mhe,Lwankomezi amesema kuwa Futari hiyo ni Mchele pamoja na Sukari na walengwa ni waamini wote ambao wapo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni desturi yake yenye lengo la kuwafariji, kuleta umoja, upendo na mshikamano katika jamii.
Katibu wa Bakwata Wilaya ya Bukoba Vijijini Ndg,Ahmed Baitu amemshukru kwa Futari hiyo na kumsihi kuendelea kuikumbuka jamii yake.
Aidha naye Imam wa Msikiti wa Katoma Ndg,Yakub Abdallah Bishazo amesema kuwa kwa alichokifanya Dkt Rweikiza ni ishara ya kujali hivyo wanamuombea kwa mwenyezi mungu ili mambo yake yaendelee kuwa mepesi huku Mwenyekiti wa Vijana Bakwata Bukoba Vijijini Ndg,Shafi Abudkadri Kwa niaba ya vijana amemshukru sana Mbunge huyo.
Social Plugin