Benki ya CRDB katika mwendelezo wake wa kuwafuturisha wadau wake katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan imekutana na wateja pamoja na viongozi wa dini na Serikali na kuwafuturisha katika ukumbi wa Nitesh Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Mbali na kufuturisha benki ya CRDB imetoa vyakula na vitu mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Hope Orphanage Center kilichopo Manispaa ya Kahama.
Mgeni rasmi katika tukio hilo lililofanyika Aprili 5,2024 alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ambaye ameipongeza benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa karibu na jamii na kuwajali wenye uhitaji kama walivyofanya kwa kituo cha New hope Orphanage Center.
Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana amewaomba waislamu na hata wasio waislamu kuchangamkia huduma za AL BARAKAH ikiwemo akaunti na mikopo inayofuata misingi ya dini ya kiislamu.
Vile vile amewahimiza waalikwa wote kuendelea kutumia huduma ya BIMA inayofuata sharia (TAKAFUL) ambayo imeanza kutolewa na benki ya CRDB hivi karibuni kwa kushirikiana na Zanzibar Insurance Corporation (ZIC)
Social Plugin