Katika hali isiyo ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Sunday mkazi wa kitongoji cha Misungwi kata ya Usagara wilaya Misungwi Jijini Mwanza anatuhumiwa kubaka kuku hadi kufa.
Wakizungumza na EATV baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtuhumiwa alimkamata kuku huyo ambaye alikuwa anataga kisha kumuingiza ndani ya nyumba yake na kuanza kumbaka na baada ya kumaliza haja zake alienda kumtupa nje.
Delifina Boazi ni mmoja wa wapangaji katika nyumba hiyo amesema alitoka nje kwenda kukinga maji bombani ndipo alipomuona mtuhumiwa akifanya kitendo hicho sebleni akiwa amekaa kwenye makochi
"Nilimuoma alikuwa amemkamata kuku na anafanya naye mapenzi na alipomaliza alienda kumtupa," amesema Delifina.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kitongoji cha Misungwi, Samson Madirisha amekiri kupokea taarifa hizo na baada ya kufika eneo la tukio alikuta kitendo hicho kufanyika.
Madirisha amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa alikuwa na hamu hivyo alishindwa kujizuia.
Naye Kamanda wa Sungusungu kata ya Usagara, Buhili Makubilo na mkazi wa eneo hilo Edista Mganga wameviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu wanaobainika kufanya vitendo hivyo.
Hata hivyo polisi wilaya ya Misungwi wamefika kwenye nyumba ya mtuhumiwa na kumchukua kwa ajili ya mahojiano zaidi. Chanzo EastAfricaTV
Social Plugin