MBUNGE BYABATO : MIRADI MINGI IMETEKELEZWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 3 YA RAIS SAMIA

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato akizungumza na wananchi .

Na Mariam Kagenda - Kagera

Katika kipindi cha miaka 3 ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Manispaa ya Bukoba imepokea kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa hiyo .

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Adv Stephen Byabato amesema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Jimbo la Bukoba mjini ambao umefanyika maeneo ya Soko kuu lililopo katika Manispaa hiyo.


Mhe.Byabato amesema kuwa katika miaka 3 ambayo imefikiwa mwaka huu ya serikali ya awamu ya 6 ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zaidi ya shilingi Bilioni 15 zimeletwa kutoka serikali Kuu na nyingine zimekusanywa na Manispaa ambapo fedha hizo zimetumika katika shughuli mbalimbali.


Amesema kuwa kupitia fedha hiyo mambo mengi yamefanyika katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali katika elimu msingi na Sekondari,Afya,Barabara,Viwanda,Biashara na uwekezaji pamoja na maendeleo mengine kama hayo ambayo yamefanyika katika kila kata na wananchi wameyaona hivyo amewahimiza viongozi walioko katika maeneo hayo kuendelea kuyazungumzia na kuyaeleza kwa wananchi ili kwa ambao hawayafahamu waweze kufahamu kilichofanyika katika miaka 3 ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Ametaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa kipindi hicho kwa uchache kuwa ni pamoja na uwekaji wa yaa za barabarani, marekebisho katika Soko kuu,usafishaji wa mto Kanoni,ujenzi wa shule mpya za Msingi na Sekondari , uboreshaji wa miundombinu ya Madarasa,Hospitali ya wilaya iliyopo Nshambya ,Ujenzi wa Zahanati ,ufunguaji wa Barabara kila eneo pamoja na ufungaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na kuongeza kuwa yapo mambo mengine mengi mazuri yanayotarajiwa kutekelezwa katika manispaa hiyo.


Ameongeza kwa kuwahimiza wafanyabiashara wa soko kuu kuwa watulivu kwani taratibu zitakapokamilika watapewa taarifa na kuwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post