Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa MNEC Leonard Mahenda Qwihaya amekuwa Mgeni Rasmi katika Fainali ya Ramadhani cup iliyo hitimishwa jana katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kirumba jijini Mwanza.
Fainali iyoo ilikutanisha Timu Mbili ambazo ni Godon Fc Vs Mamlaka Fc ambapo Timu ya Godon Fc imeweza kuibuka na Ushindi wa goli 3 kwa Mamlaka Fc 0 Ivo basi Timu ya Godon Fc ni Mabingwa wa Ramadhani cup 2024
Mnec pia aliongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Kata jirani pamoja na Katibu wa UVCCM Mkoa Joshua Ramadhani MNEC Qwihaya alitumia fursa hiyo kuwataka Vijana kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri. anazozifanya
Qwihaya aliongoza Maandamano ya Amani kutoka Ofisi za CCM Kata ya Kirumba kuelekea uwanja wa Shule ya Msingi Kirumba
Social Plugin