Ahadi hiyo ya Mkondya ambaye ni mdau mkubwa wa michezo imekuja siku chache tu baada ya juzi kutoa ahadi ya kuwapa Dodoma Jiji Nguruwe ama shilingi laki saba kwa kila goli ambalo wangelifunga dhidi ya Yanga Sc lakini bahati mbaya hawakufunga hivyo kukosa zawadi hiyo.
"Juzi nilitoa ahadi ya kuwapa Dodoma Jiji Nguruwe mwenye thamani ya shilingi laki saba kwa kila goli ambalo wangelifunga dhidi ya Yanga Sc bahati mbaya hawakufunga hivyo kukosa zawadi hiyo nawapa pole sana.
Sasa mimi pia ni shabiki wa timu ya Simba Sports Club, na timu yetu kwa sasa inapitia wakati wa ngumu wa upatikanaji matokeo tumefungwa mechi tatu mfululizo na Al Ahly nje ndani na kutolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, pia tukafungwa na Mashujaa na kutolewa katika michuano ya Shirikisho Tanzania hii ni aibu kwetu",amesema Mnkondya.
"Sasa ili kuwapa motisha katika mchezo wa kesho dhidi ya Ihefu ama kama inavyofahamika sasa kama Singida Black Stars mimi na Kampuni yangu tunaahidi kutoa Nguruwe mmoja mkubwa aina ya Large White mwenye kilo 500 kwa kila goli litakalofungwa na Simba katika mchezo huo au kiasi cha Tsh. Milioni 3 ambayo ni thamani ya Nguruwe huyo.
Lakini pale simba kuna watu wawili wanafanya kazi sana na hao napenda kuwapa zawadi ya Nguruwe kama tutashimda mchezo wa kesho ambao ni Msemaji Ahmed Ally na Mchezaji Clatous Chama hawa wanapambana sana",amesema Mnkondya.
Mradi wa Kijiji cha Nguruwe upo Zamahero Dodoma Zamahero, ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakifika hapo kuwekeza ili kuinua uchumi, michezo nk.
WASILIANA na Kijiji cha Nguruwe +255 756 000 095
Social Plugin