Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi cheti cha udhamini Bi. Lulu Mengele, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, kwa kuwa miongoni mwa wadhamini wa Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), uliofanyika tarehe 29 Aprili, 2024 jijini Dodoma.
Katika mkutano huo ambao uliofunguliwa na Mhe. Dkt. Biteko, amesema Serikali ya awamu ya sita inathamini mchango mkubwa unaotolewa na vyombo vya habari nchini.
Akitoa elimu ya hifadhi ya jamii katika mkutano huo, Bi. Lulu Mengele amesema NSSF inaendelea kufanya vizuri kwenye sekta ya hifadhi ya jamii na kuwa imeboresha mifuko ya TEHAMA ambayo ni rahisi na rafiki kwa wanachama ambao wanaweza kuangalia taarifa zao mbalimbali zikiwemo za michango bila ya kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.
Aidha, amewataka waajiri wa sekta binafsi kuhakikisha wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao kila mwezi kwani hilo ni takwa la kisheria.
Social Plugin