Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TCRA YAHAMASISHA UCHUMI WA KIDIGITALI, YATAHADHARISHA PICHA CHAFU FACEBOOK 'KESI ZA UTAPELI MTANDAONI ZIPELEKWE POLISI'

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka Watanzania kuendelea kujihabarisha, kuhamasishana na kutumia huduma za Kidigitali ili kufikia Uchumi wa Kidijitali huku ikisisitiza matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Rai hiyo imetolewa leo Jumanne Aprili 9,2024 na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Huduma za Mawasiliano ikiwemo
uelewa wa majukumu ya TCRA, Masuala ya maadili ya vyombo vya habari na uelewa kuhusu Kanuni za utangazaji wakati wa Uchaguzi.

Mhandisi Imelda amesema kutokana na kwamba Sekta ya Mawasiliano inakua na kufungua fursa mbalimbali hivyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuwekeza kwenye Sekta ya Mawasiliano ili kufikia uchumi wa Kidigitali na kuleta mchango kwenye maendeleo ya nchi.

“Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 idadi ya watu waliopo Tanzania ni Milioni 61. Hadi kufikia Desemba 2023 idadi ya Laini zilizosajiliwa ni Milioni 70.3, watumiaji wa Intaneti ni Milioni 35.8 na Akaunti za Pesa Mtandao ni Milioni 52.9. Kutokana na takwimu hizi ni vyema tukaendelea kuhamasishana kuhusu matumizi ya huduma za kidigitali ili kufikia uchumi wa kidigitali”,ameeleza Mhandisi Imelda.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum.

“Tupo katika ulimwengu wa Kidigitali, uchumi wa kidigitali, Lengo la TCRA ni kuwapeleka Wananchi katika uchumi wa kidigitali hivyo tunahitaji wadau wafahamu kuhusu uchumi wa kidigitali kwa kutumia huduma zinazoendeshwa kupitia mtandao, tuendelee kuhamasisha na kuhabarisha wananchi watumie huduma za kidigitali ili kupata huduma”,ameongeza Mhandisi Imelda.

Katika hatua nyingine, kesi za Uhalifu Mtandaoni ukiwemo wizi na utapeli katika mazingira ya mtandaoni, zisipelekwe TCRA bali zinapaswa kupelekwa Jeshi la Polisi kwa sababu Polisi ndiyo wamepewa jukumu la kushughulika na uhalifu.

“TCRA inafanya kazi zake kwa ukaribu sana na Jeshi la Polisi ambalo lina dhamana kwa mujibu wa sharia kulinda usalama wa watu na mali zao. Kupitia sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 jeshi la Polisi linasimamia masuala ya usalama wa mtandao na kushughulika na uhalifu mtandaoni. TCRA inashirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa elimu kwa umma kuhusu uhalifu mtandaoni na matumizi salama ya huduma za mawasiliano”,amesema Mhandisi Imelda.

Pia ametahadharisha kuhusu matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii akitaka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa makini huku akiwataka watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaokumbana na vitendo vya uhalifu kama vile kuhusishwa (Tag) na picha chafu katika mtandao wa Facebook watoe taarifa polisi ili wahalifu wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015.

"Tuwe makini tunapotumia mitandao ya kijamii, usiweke taarifa zako nyingi mtandaoni,ni vizuri kujua kuhusu masuala ya usalama mtandaoni, usalama unaanza na wewe. Epuka kuweka kila kitu mtandaoni na pindi unapopata changamoto ikiwemo hizi za utapeli toa taarifa kwa mtoa huduma wako", amesema.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa wito kwa wanataaluma ya habari kuchukua tahadhari na kuwa makini wakati wanapotoa taarifa zinazohusu masuala ya Uchaguzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru ameishukuru TCRA kutoa semina elekezi kwa waandishi wa habari hali ambayo itasaidia kuboresha huduma za mawasiliano.

Naye Mwezeshaji Edwin Soko amewataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi wa habari ili kuwa salama kwa kuepuka kuweka hisia, kushabikia, chuki, rushwa na kufuata sheria za nchi.

Akiwasilisha mada kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa baadae mwaka huu na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao, Afisa Mawasiliano wa TCRA Robin Albert Ulikaye alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuzingatia Kanuni za Utangazaji wakati wa Uchaguzi ili kuhakikisha uwasilishaji wa habari unafuata kanuni za utangazaji wa televisheni, redio na maudhui Mtandaoni.

“Ndugu wanataaluma napenda kuwakumbusha kwamba wakati tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ni muhimu taratibu za hizi Kanuni za maudhui ya utangazaji wakati wa Uchaguzi mkazizingatia,” amesisitiza.

TCRA imetoa semina elekezi kwa waandishi wa habari katika mkoa wa Shinyanga, semina iliyotanguliwa na semina nyingine iliyofanyika Jumatatu Aprili 8, 2024 mkoa wa Simiyu, ikitarajia kuhitimisha semina hizo katika mkoa wa Mara.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Aprili 9,2024- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akizungumza wakati wa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza wakati TCRA ikitoa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza wakati TCRA ikitoa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Mwezeshaji Edwin Soko akizungumza wakati TCRA ikitoa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga

Afisa Mawasiliano wa TCRA Robin Albert Ulikaye akizungumza wakati TCRA ikitoa warsha ya TCRA kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com