SHINYANGA PRESS CLUB KINARA UTEKELEZAJI MIRADI YA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga (WFT-Trust)Glory Mbia akizungumza wakati wa mafunzo hayo - Picha na Kadama Malunde

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KLABU ya Waandishi wa habari mkoani Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), imepongezwa katika miradi yake ambayo imekuwa ikiitekeleza kwa miaka Mitatu Mfululizo katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kwa kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, na kusaidia kupunguza ukatili wilayani humo.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 17,2024 na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edmund Ardon, akimwakilisha Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wilayani humo, kwenye kikao cha wadau wa ukatili pamoja na kupokea na kujifunza juu ya utafiti wa Citizen For Change na Women Fund Tanzania, kikao kilichoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Shinyanga kwa ufadhili wa WFT-Trust.

Amesema Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga inawapongeza wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwamo Waandishi wa Habari,kwa kuendelea kutekeleza Miradi ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa Kijinsia ndani ya jamii kwa kusaidiana na Serikali katika utekelezaji wa mpango wa (MTAKUWWA) na kuleta ukombozi kwa wanawake na watoto.

“Tunawapongeza Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga ambapo kupitia Miradi yenu mmekuwa Mkiibua na kufichua vitendo vya ukatili ambavyo vinatendeka ndani ya jamii, na kuvikemea kwa kutumia Kalamu zenu pamoja na kuelimisha pia, ambapo matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yamepungua kwa kiasi kikubwa wilayani Shinyanga,”Amesema Ardon.

“Serikali halmashauri ya wilaya ya Shinyanga tutaendelea kushirikiana na Wadau wa Maendeleo pamoja na Waandishi wa habari, juu ya Miradi yenu ambayo mmekuwa mkiitekeleza ili kumaliza kabisa vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuleta usawa ndani ya jamii,”Ameongeza Ardon.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, amesema waandishi wa habari wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuibua,kubaini na kutoa taarifa za ukatili hadharani na kisha viongozi kuchukua hatua.

“Ukatili kwa wanawake na watoto bado upo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,ambapo tunahitaji nguvu ya pamoja kwa kushirikiana na wadau na Waandishi wa Habari katika kutokoneza ukatili huu wa Kijinsia,”amesema Mboje.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust)mkoani Shinyanga Glory Mbia, amesema tangu mwaka 2019 wamekuwa wakitoa Ruzuku kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ndani ya jamii na kuonyesha kuridhishwa na matokea ya kupungua kwa ukatili.

Amesema Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wamekuwa Chachu kubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Serikali wa (MTAKUWWA), na wameonyesha Jinsi gani Waandishi wa habari walivyo na nguvu katika kuleta mabadiliko ndani ya jamii.

“Waandishi wa habari zamani tulikuwa kuliwachukulia ni watu wa kuandika habari za kukosoa tu, lakini ninyi Waandishi wa habari hapa Shinyanga mmeondoa Mtazamo huo, ambapo kupitia Miradi yenu mmekuwa mkiandika habari chanya na zenye kuleta mabadiliko ndani ya jamii, na sisi kama WFT tutaendelea kufanya kazi na ninyi, Serikali na NGO,”Amesema Glory.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, ameupongeza Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust), kwa kuendelea kushirikiana nao na kuwapatia Ruzuku ya kutekeleza miradi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema ndani ya miaka mitatu mfululizo ya utekelezaji wa Miradi hiyo, wameweza kuandika habari 355 ambazo zimeleta mabadiliko chanya ndani ya jamii na kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia wilayani Shinyanga.

“Mwaka huu 2024 Klabu yetu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, tunatekeleza Mradi tena wilayani Shinyanga unaoitwa “Wanajamii na Vyombo vya habari katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto” kwa miezi Sita, na utagusia maeneo ya MTAKUWWA na maeneo 17 ya malengo endelevu ya mwaka 2030 kwa kutazama Jicho la Mwanamke na Mtoto,”Amesema Kakuru.

Aidha,amesema Klabu hiyo ya Waandishi wa habari Shinyanga katika kuendelea mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye maeneo mengine ya Mikoa mbalimbali wameweza kufanikiwa kaunzisha Mtandao wa Waandishi wa Habari za Ukatili Tanzania (TAJOGEV) ili kusaidia utekelezaji wa MTAKUWWA.

Pia, ametoa wito kwa Serikali pamoja na Mashirika mbalimbali ambayo yanatoa Ruzuku,washirikiane na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, kwa kuwapatia Ruzuku katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali sababu wanauwezo Mkubwa katika Uandishi wa habari zenye kuleta Mabadiliko chanya ndani ya jamii.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga (WFT-Trust)Glory Mbia akizungumza wakati wa mafunzo hayo - Picha na Kadama Malunde
Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania Mkoani Shinyanga (WFT-Trust)Glory Mbia akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza wakati wa mafunzo hayo

Mwenyekiti wa Muungano wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Ending Violence Against Women and Children Working Group -EVAWC), Jonathan Manyama Kifunda akielezea namna EVAWC inavyofanya kazi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Edmund Ardon akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngassa Mboje akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngassa Mboje akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Kikao cha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post