Na Suzy Luhende - Shinyanga
Waandishi wa habari wanawake Mkoani Shinyanga (Shy Women's Journalist) wamezindua rasmi Umoja wao kwa ajili ya kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kusaidiana katika shida na raha, ikiwa ni pamoja na kutembelea watu wenye mahitaji maalumu, yatima na wajane.
Uzinduzi huo umefanyika Mjini Shinyanga kwa lengo la kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia taaluma yao kwa kuibuwa na kuanzisha miradi itakayowawezesha kujikwamuwa kiuchumi na kusaidiana katika shida na raha na kutumia fursa mbalimbali zilizopo.
Mwenyekiti wa Chama hicho cha Waandishi wa habari wanawake Shinyanga Moshi Ndugulile, amesema umoja huo utasaidia kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo, kutembelea watoto yatima, wazee na makundi yenye mahitaji maalumu pamoja na kupata uzoefu kutoka kwa wanawake ambao wamefanikiwa zaidi.
"Sisi waandishi wa habari wanawake Mkoa wa Shinyanga tumeamua kuanzisha umoja wetu kwa ajili ya kushirikiana masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kutembea watu wenye mahitaji maalumu, kwani sisi wanawake ni jeshi kubwa tunaweza kufanya mambo makubwa katika jamii yetu", amesema Ndugulile.
Katibu wa Chama hicho, Stella Ibengwe,amewaomba waandishi wa habari wanawake kuimarisha umoja wao hatua ambayo itawawezesha kupiga hatua zaidi na kuwa na mafanikio makubwa,huku akiwapongeza kwa hatua hiyo ya uzinduzi kwani ni njia ya mafanikio.
Baadhi ya wajumbe wa Umoja huo akiwemo Elizabeth Charles na Suzy Butondo wamewaomba waandishi wanawake wadumishe upendo katika umoja wao, huku wakimtegemea Mungu aweze kuwasimamia kwa kila jambo wanalotaka kulifanya ili liweze kufanikiwa.
"Leo tumezindua Umoja wetu kwa pamoja, hivyo niwaombe tushirikiane kwa pamoja na tumshirikishe Mungu aweze kutusimamia kwa kila jambo tunalotaka kulifanya