Watu wawili jinsi ya kike wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wameuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka miwili kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao.
Waliouawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani na Mkazi wa Kiwanja kata ya Kiwanja Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na mwingine ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.
Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni Machi 31,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.
Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje.
Akizungumza na EATV Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiwanja mahali alipokuwa akiishi mwalimu huyo Gideon Peter Kinyamagiha amesema walifika nyumbani kwa marehemu na walipoingia ndani walikuta sururu ikiwa na damu na marehemu wawili na mtoto wa kiume wa mwalimu huyo akiwa amejuriwa uongozi ulitoa
Kinyamagoha anasema baadaye walitoa taarifa Polisi ambao nao walifika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua miili na kwenda kuihifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi ambapo majeruhi amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.
Tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamtafuta mtu/watu waliohusika katika tukio hilo la mauaji ya aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Heriety Lupembe (37) na Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Isenyela Ivon Tatizo (15) wote wakazi wa Kijiji cha Kiwanja Wilaya ya Chunya
SACP Benjamin Kuzaga
Kwa Mujibu wa taarifa ya jeshi la Polisi SACP Benjamin Kuzaga inaeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 31, 2024 majira ya saa 2:30 usiku wakati marehemu akiwa nyumbani kwake sebuleni na watoto wawili Ivon Tatizo na Haris Barnaba Mtweve (06) Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Mchepua wa kiingeleza ya Ken Gold aliyejeruhiwa kwa kupigwa kitu butu kichwani.
Kamanda Kuzaga Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, mtu huyo aliwavamia marehemu na kuanza kuwashambulia na baada ya kufanya hivyo alifunga milango kwa nje na kuondoka na funguo.
Chanzo cha tukio hili bado kinachunguzwa.
Majeruhi mtoto Haris Mtweve anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni Pamoja na msako dhidi ya mtu au watu waliohusika.
Aidha, linatoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa za mtu au watu waliohusika katika tukio hili kutoa taarifa ili wakamatwe.
CHANZO - EATV