VIJANA 58 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI VIHENGE KUPITIA MRADI WA TANIPAC KUZUIA SUMUKUVU

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jumla ya Vijana 58 kutoka mikoa ya Tabora, Mwanza, Geita na Simiyu wamehitimu mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa ‘Tanzania Initiative For Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo wenye lengo la kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi na kuimarisha afya ya jamii.

Akizungumza leo Ijumaa Aprili 26,2024 wakati wa kufunga Mafunzo ya kutengeneza Vihenge awamu ya tatu, Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban amesema mafunzo hayo yamehitimishwa rasmi baada ya kutolewa katika awamu tatu yakinufaisha vijana 58.

“Mafunzo ya kutengeneza vihenge yalianza tarehe 26,2024 kwa awamu ya kwanza ambapo washiriki walikuwa 19, ikafuatia awamu ya pili ikiwa na washiriki 23 na leo washiriki 16 wamehitimu. Wamefundishwa masuala ya ujasiriamali, utengenezaji wa vihenge kwa nadharia na vitendo, nadharia ya masoko, usimamizi wa fedha na urasimishaji wa biashara”,amesema Taban ambaye ni Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga.

“Serikali kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi na kuimarisha afya ya jamii. Mradi wa TANIPAC unalenga kuwezesha jamii kutumia njia sahihi na za kisasa za uhifadhi wa nafaka hususani mahindi kutokana na sumukuvu”,ameongeza Taban.

Amefafanua kuwa, Serikali imeingia gharama kuhakikisha kuwa vijana wanapatiwa ujuzi wa kutengeneza vifaa vya kisasa na vinavyodumu kwa muda mrefu (vihenge) ili kutimiza adhima ya kupunguza sumukuvu.

Taban amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanayatumia kwa vitendo kuhakikisha kuwa lengo la mafunzo linatimia ambapo pia yatawezesha kuongeza kipato cha mmoja mmoja, kaya na taifa kwa ujumla.

“Mafunzo haya yametolewa kwa vijana wachache lakini wengi wangependa kupata mafunzo haya,hivyo nitumie nafasi hii kuwaomba mkawe waalimu wa kufundisha vijana wenzenu kwenye maeneo yenu ya kazi ili kwa pamoja tuweze kupambana kwa vitendo kupunguza kama siyo kuondoa kabisa sumukuvu”,amesema Taban.

Akisoma risala kwa niaba ya Washiriki wenzake wa mafunzo, Wanjala Daudi amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji kazi na kuzalisha bidhaa za vihenge (Silos) na nyinginezo kwa tija ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

“Tunaushukuru uongozi wa SIDO na Wizara ya Kilimo kwa kutoa fursa ya mafunzo haya. Hakika mafunzo haya yametujengea uwezo wa kujiamini na kuamsha ari ndani yetu ya kujiajiri na kuachana na kasumba ya kusubiri ajira”,amesema Daudi.

“Pamoja na ari na motisha ya kujiajiri iliyojengeka ndani yetu, tunakabiliwa na changamoto ya mitaji kwa ajili ya kununua vifaa/vitendea kazi vya kuanzisha shughuli mbalimbali kutokana na fani tulizojifunza”,ameongeza Daudi.

Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa vijana wakati akikagua Vihenge vilivyotengenezwa na Vijana walioshiriki mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa ‘Tanzania Initiative For Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo - Picha na Kadama Malunde 1 blog
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban (kulia) akikagua Vihenge vilivyotengenezwa na Vijana walioshiriki mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban (kushoto) akikagua Vihenge vilivyotengenezwa na Vijana walioshiriki mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban (wa nne mbele kushoto) , viongozi wa SIDO Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu walioshiriki mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo

Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban akizungumza wakati wa akifunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo wenye lengo la kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi na kuimarisha afya ya jamii.
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban akizungumza wakati wa akifunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo

Mratibu wa Mafunzo ya Kutengeneza Vihenge Mkoa wa Shinyanga, Misuka Makwaya ambaye ni Mhasibu wa SIDO Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge
Mratibu wa Mafunzo ya Kutengeneza Vihenge Mkoa wa Shinyanga, Misuka Makwaya ambaye ni Mhasibu wa SIDO Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge
Wanjala Daudi akisoma risala ya washiriki wa mafunzo ya kutengeneza Vihenge
Afisa Mipango SIDO Shinyanga , Frank Nguyu akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge
Mwenyekiti wa Mafunzo, Charles Kulwa akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge
Mratibu wa Mafunzo SIDO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Manyama Lububi akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge

Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban (kulia), akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki mafunzo ya kutengeneza Vihenge 

Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bw. Joseph Taban, viongozi wa SIDO Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu walioshiriki mafunzo ya kutengeneza Vihenge yaliyotolewa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia Mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post