Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANROADS YAKUTANA NA WADAU WA USAFIRI WA ANGA.. UJENZI UWANJA WA NDEGE SHINYANGA WASHIKA KASI

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mkoa wa Shinyanga  umewakutanisha wadau mbalimbali wa usafiri wa anga kutoka taasisi za serikali na binafsi kwa lengo la kujadili maendeleo na fursa kwa wananchi katika uwanja wa ndege uliopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Akitoa  taarifa leo Jumatano Aprili 17,2024 Mhandisi wa Mradi wa uwanja wa Ndege Shinyanga kutoka TANROADS, Binemungu Donatus amesema kwa kuzingatia shughuli zote ambazo zimefanyika katika ujenzi, mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 12.07.

Amesema ujenzi wa njia ya kuruka na kutua ndege imefikia asilimia 40.3, barabara ya kiungo imefikia asilimia 40, eneo la maegesho limekamilika kwa asilimia 40 huku ofisi ya mhandisi imekamilika kwa asilimia 100.

Amesema zaidi ya watanzania 100 wakiwemo wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wameajiriwa katika mradi huo.

“Mradi huu umetoa jumla ya ajira 112 ambapo ajira 96 sawa na asilimia 86 zimetolewa kwa watanzania, changamoto kubwa inayokwamisha utekelezaji wa mradi huu ni mvua nyingi zinazoendelea kunyesha kwa sababu Mvua ikinyesha tunasubiria kuanzia siku tatu ardhi ikauke kwanza ndiyo tunaendelea ikiwa inashenye kila siku inakwamisha sana lakini pia tulipata changamoto ya ucheleweshwaji wa uhamishaji huduma za maji pamoja na miundombinu ya umeme kutoka eneo la mradi”, amesema Mhandisi Donatus.

“Mradi huu ukikamilika utarahisisha usafiri kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga, Simiyu na Mikoa ya jirani lakini pia utarahishaji shughuli za kibiashara hasa uchimbaji madini, ufugaji na kilimo pia utawezesha shughuli mbalimbali za kijamii lakini pia mradi huu utasaidia sana kukuza uchumi wa Mkoa wa Shinyanga na Simiyu, utasaidia shughuli za utafiti wa kilimo pamoja na kukuza utalii katika Mkoa wa Shinyanga, Mikoa jira na Taifa”,amesema Mhandisi Donatus
Kaimu Meneja TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel amesema uwanja wa ndege Shinyanga kwa hatua za awali utaanza kutumika kuanzia Mwezi Agosti,2024 na kwamba mkandarasi anaratajiwa kukamilisha Mwezi Oktoba Mwaka huu 2024 ambapo gharama ya mradi ni Bilioni 44.8.

Mhandisi Joel ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika mradi huo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuchangamkia fursa zilizopo.

“Ujenzi unaenda vizuri sana kwa kasi jengo letu linaendelea vizuri na tunatarajia uwanja wetu wa Ndege utaanza kutumika kwa hatua za awali kuanzia Mwezi wa nane mwanzoni lakini ujenzi utakuwa unaendelea kufikia Mwezi wa kumi tunatarajia mkandarasi awe ameshakamilisha shughuli zote za uwanja wa Ndege Shinyanga”,amesema.

“Niendelee kuishukuru serikali inayoongozwa na Mama yetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoendelea kuleta fedha na kufungua fursa katika Mkoa wa Shinyanga na sisi tutahakikisha hii miundombinu inajengwa kama inavyokusudiwa na ile thamani ya fedha inaonekane ili uchumi wa Shinyanga na taifa kwa ujumla uendelee kuimarika, niendelea kutoa rai kwa wananchi kwamba huu mradi una fursa nyingi sana ambazo zipo kipindi cha ujenzi lakini pia hata baada ya kukamilika kwa ujenzi niwaomba hasa wakazi wa Shinyanga wajitokeze kupokea hizo fursa”,amesema Mhandisi Joel.

Wadau mbalimbali kutoka kwenye taasisi za serikali na taasisi binafsi wamepongeza kwa hatua iliyofikiwa katika ukarabati na uboreshaji wa uwanja wa Ndege wa Shinyanga ambapo wameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hilo kwa la kutoa fursa kwa wananchi.

Mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga unaojengwa na Mkandarasi China Hennan International Corperation Group Co. Ltd (CHICO) na unaosimamiwa na Wakandarasi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia umeanza Aprili 4,2023 na unatarajia kukamilika ifikapo Oktoba 3,2024 (ndani miezi 18) ukijengwa kwa fedha za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mkopo kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB).
Viongozi na wadau mbalimbali kutoka kwenye taasisi za serikali na binafsi wakisikiliza maelezo ya hatua za mradi wa ukarabati na uboreshaji wa uwanja wa Ndege wa Shinyanga, leo Aprili 17,2024.
Viongozi na wadau mbalimbali kutoka kwenye taasisi za serikali na binafsi wakisikiliza maelezo ya hatua za mradi wa ukarabati na uboreshaji wa uwanja wa Ndege wa Shinyanga, leo Aprili 17,2024.
Viongozi na wadau mbalimbali wakitembelea Mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga
Viongozi na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na taasisi binafsi wakiendelea kutembelea mradi Mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga

Mhandisi wa mradi wa uwanja wa Ndenge Shinyanga, kutoka TANROADS , Binemungu Donatus akieleza hatua mbalimbali za mradi wa ukarabati na uboreshaji wa uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mhandisi wa mradi wa uwanja wa Ndenge Shinyanga, kutoka TANROADS , Binemungu Donatus akieleza hatua mbalimbali za mradi wa ukarabati na uboreshaji wa uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Kaimu meneja TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel Mwambugu akizungumza kwenye kikao cha pamoja na wadau mbalimbali wa usafiri wa anga
Viongozi na wadau mbalimbali wa uwanja wa Ndege wa Shinyanga, kutoka kwenye taasisi za serikali na binafsi wakiwa katika kikao cha pamoja na TANROADS Mkoa wa Shinyanga 

Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Bi. Joyce Chagonja akitoa maoni yake kuhusu maboresho na fursa mbalimbali katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga
Afisa mahusiano kutoka NMB Benki tawi la Shinyanga akitoa maoni  kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Afisa matekelezo mkuu kutoka NSSF Mkoa wa Shinyanga Bi. Hawa Godigodi akitoa maoni yake kuhusu maboresho na fursa katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Meneja TRA Mkoa wa Shinyanga Bwana Faustine Mdessa akitoa maoni yake kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga

Beni Lucas Lihawa kutoka Karena Hotel akitoa maoni yake kuhusu maboresho na fursa katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Meneja mahusiano na biashara wateja wakati na wakubwa NBC Benki tawi la Shinyanga akitoa maoni yake kuhusu maboresho na fursa kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Mhandisi Sai Kapera kutoka KASHWASA akitoa maoni yake kuhusu maboresho na fursa katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga, kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Afisa mkuu uendeshaji NSSF Mkoa wa Shinyanga Ahmed Ally Salum akitoa maoni yake kuhusu maboresho na fursa katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Meneja wa uwanja wa Ndege wa Shinyanga Mhandisi Lugano Mwinuka akitolea ufafanuzi maoni na maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Kikao kikiendelea.
Mhandisi mkuu huduma za usafiri wa Anga Tanzania, Mpeli Ngonywike akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Meneja mamlaka ya hali ya hewa kanda ya ziwa, Augustino Nduganda akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Mhandisi mradi kutoka mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mhandisi Simon Mathias akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Nasser Elgohary kutoka kampuni ya SMEC International Ltd akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Nasser Elgohary kutoka kampuni ya SMEC International Ltd akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Meneja mradi kutoka kampuni ya China Henan International Cooperation Group Ltd (CHICO), Shi Yinlei akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Meneja mradi kutoka kampuni ya China Henan International Cooperation Group Ltd (CHICO), Shi Yinlei akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usafiri wa anga mkoa wa Shinyanga
Shughuli mbalimbali zikiendelea katika ukabarati na uboreshaji uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Shughuli mbalimbali zikiendelea katika ukabarati na uboreshaji uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Shughuli mbalimbali zikiendelea katika ukabarati na uboreshaji uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com