Msanii mkongwe nchini, Afande Sele akiwa Kilindi mkoani Tanga kwenye shamba la miche ameipongeza wizara ya kilimo chini ya Mhe. Hussein Bashe kwa maendeleo makubwa kwenye sekta ya kilimo nchini na kwa kujitoa kimasomaso kuwafikia wakulima moja kwa moja.
Afande Sele amesema kuwa ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia, Taifa limeshuhudia ongezeko kubwa la Bajeti ya Kilimo inayolenga kuongeza tija kwa Wakulima kutokana na umuhimu wa sekta hiyo kwa Taifa letu.
"Tumetoka kwenye kilimo cha kulialia na kilimo cha mahangaiko, sasa tupo kwenye kilimo biashara",aliongeza Afande Sele.
Social Plugin