Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BONANZA LA MICHEZO GUMZO KISHAPU.. KESHO FAINALI MPIRA WA MIGUU NA PETE KISHAPU KUENZI MIAKA 60 YA MUUNGANO



Kaimu katibu tawala wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bw.Given Noah akizungumzia uzalendo wa muungano wakati wa uzinduzi wa bonanza la michezo uliofanyika leo Jumanne Aprili 23,2024 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe wilayani humo.

Na Sumai Salum _Kishapu

Bonanza la michezo mbalimbali limezinduliwa leo Jumanne April 23, 2024 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanzania wilayani humo.


Akizungumza wakati wa Uzinduzi Kaimu Katibu tawala wilaya ya Kishapu Bw. Given Noah amesema michezo itakayofanyika ni pamoja na mpira wa miguu timu (4),mpira wa pete timu (3),mashindano ya wazee wa miaka 60 kukimbiza kuku pamoja na mashindano ya mchezo wa bao .

"Tunafanya haya yote kwa ajili ya kukumbuka na kuuenzi muungano wetu ambao waasisi wake hayati baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Shekkh Abeid Karume wa Zanzibar miaka 60 iliyopita walikuwa na mapenzi ya dhati kabisa kwa kutuweka pamoja kwa umoja tukawa watanzania wote bila kujali rangi,dini,taifa wala kabila na sasa tuko na mwingiliano bila zuio lolote", amesema Noah.


Aidha Aprili 23,2024 katika mpira wa miguu awamu ya kwanza wamecheza Lubaga Fc dhidi ya Ghazza fc ambapo Ghazza fc imeibuka kidedea kwa magoli 8-0 awamu ya pili wamecheza Kishapu Sekondari dhidi ya Kishapu Veteran wakatoka sale ya 2-2 na kisha Kishapu Veteran wakashinda kwa mkwaju wa penat ya 4-3.




Kwa upande wa Mpira wa pete wamechuana Isoso Sekondari dhidi ya Kishapu Sekondari na Isoso imeibuka kidedea kwa mabao 7 huku Kishapu Sekondari ikitoka na mabao 6.




Hivyo April 24,2024 itakuwa fainali kati ya Kishapu Veteran na Ghazza Fc (mpira wa miguu) na mpira wa pete watashindana Isoso Sekondari na Kishapu Veteran wanawake, huku wazee wa miaka 60 wakikimbiza kuku na kesho kutwaalhamis april,25,2024 kutamalizika sherehe za muungano kwa mkesha kukiwa na mchezo wa bao,ngoma na burudani mbalimbali katika viwanja vya shirecu wilayani humo kunzia saa 1 jioni hadi saa 6 usiku.
Kaimu katibu tawala wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bw.Given Noah akizungumzia uzalendo wa muungano wakati wa uzinduzi wa bonanza la michezo uliofanyika leo Jumanne Aprili ,23,2024 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe wilayani humo.
Wachezaji wa Lubaga Fc kutokea wilayani Kishapu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mchezo waliotoka 0-8 dhidi ya Ghazza Fc mashindano yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe kuelekea madhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanzania
Wachezaji wa Ghazza Fc kutokea wilayani Kishapu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ushindi wa 8-0 dhidi ya Lubaga Fc mashindano yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe kuelekea madhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanzania
Baadhi ya Wachezaji wa mpira wa pete kutoka timu ya Isoso Sekondari na Kishapu Sekondari wakicheza leo April 23,2024 katika viwanja vya Buduhe Shule ya msingi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambapo Isoso imeichapa KIshapu bao 7-6 na hivyo  Aprili 24,2024 itacjeza fainali na Kishapu Veteran wanawake kuelekea maadhimisho ya miaka 60 yw muungano
Kikosi cha Kishapu Sekondari kikisikiliza maelekezo kutoka kwa Afisa utamaduni Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Queen Mwajilala wakati wa uzinduzi wa bonanza la michezo leo Aprili 23,2024 yaliyofanyika katika viwanja vya michezo Shule ya msingi Buduhe kuelekea maadhimisho  ya miaka 60 ya muungano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com