Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking News : AMOS MAKALLA ABEBA MIKOBA YA MAKONDA CCM, MONGELA AMRITHI ANAMRINGI MACHA, HAPI APELEKWA WAZAZI, JOKETI UVCCM



Amos Makala
John Mongella

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 03 Aprili, 2023 jijini Dar es Salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuwachagua wajumbe kama ifuatavyo:-,

i. Ndugu John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Ndugu Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

ii. Ndugu Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Ndugu Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

iii. Ndugu Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, akichukua nafasi ya Ndugu Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,

iv. Ndugu Jokate Urban Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, akichukua nafasi ya Ndugu Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dkt Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
IMETOLEWA NA IDARA YA ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO
03 APRILI, 2024

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com