Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameagiza wakandarasi kukamilisha ujenzi Machi mwakani na kwa ubora unaotakiwa. Ujenzi wa uwanja huo utakaogharimu zaidi ya sh. Bil. 60 utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 150, 000 kwa mwaka na utarahisisha zaidi usafiri kwa wakazi na wageni.
Watu 120 wamepata ajira katika mradi huo ambapo wazawa wamekuwa 114.
Dkt. Nchimbi ametoa maagizo hayo leo Aprili 15, 2024 wakati kiwaongoza viongozi wa chama na serikali kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga kwenye ziara yake mkoani Rukwa
Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea kesho katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.
Social Plugin