Na Dotto Kwilasa,DODOMA
WAZIRI Wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax , amesema wizara yake kupitia JWTZ imechangia katika kulinda mipaka ya nchi pamoja na kujenga uchumi imara ambao umepelekea wananchi hujishughulisha na uzalishaji mali bila hofu.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi Wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Amesema kwa kipindi cha miaka 60 ya muungano Serikali kupitia Wizara hiyo imeendelea kutekeleza, na kuliimarisha Jeshi kwa kulipatia zana na vifaa bora na vya kisasa, rasilimali watu, na nyenzo za kufanyia mazoezi ili kuwa imara wakati wote.
"Mchango mwingine mkubwa wa Jeshi hilo katika miaka 60 ya Muungano, ni ulinzi madhubuti wa mipaka yetu, uhuru, na katiba. Nchi imeendelea kuwa imara na yenye amani katika awamu zote;
Pia , katika miaka 60 ya Muungano, Wizara ya Ulinzi na JKT Pamoja taasisi zake zimeendelea kufanya na kuendeleza tafiti na uhawilishaji wa teknolojia kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia, "ameeleza Waziri huyo wa ulinzi.
Licha ya hayo ametaja mafanikio mengine ya muungano kuwa ni pamoja na Serikali kuanzisha viwanda vya kijeshi likiwemo shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) maarufu kama NYUMBU, pamoja na Shirika la MZINGA.
"Katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, serikali kupitia wizara ya Ulinzi na JKT, imeendeleza pia kudumisha uhusiano na mataifa mbalimbali duniani, kupitia mafunzo na mazoezi ya kijeshi, misaada ya kitaalam, vifaa, zana na mitambo,
Pamoja na hayo tumefanikiwa pia kupitia ubadilishanaji wa wataalam, ubadilishanaji taarifa za uhalifu unaovuka mipaka, shughuli za ulinzi wa amani, mapambano dhidi ya ugaidi, uharamia baharini, uvuvi haramu, na usafirishaji haramu wa binadamu, .
Social Plugin