Na Sumai Salum - Kishapu
Bonanza la michezo ya mpira wa miguu,pete na kukumbiza kuku limehitimishwa April 24,2024 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Buduhe Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.
Kufuatia mashindano hayo yaliyofunguliwa jana na Kaimu Katibu Tawala Bw.Given Noah na kufungwa leo na Msimamizi mkuu wa sherehe za Muungano wilayani humo Mhe.Joseph Mkude Ghazza Fc imechuana na Kishapu Veteran huku Ghazza ikiibuka kidedea kwa bao 1-0 katika kipindi cha pili na mpira wa pete,Kishapu Veteran kujipatia ushindi kwa mbinde wa mabao 8-5 dhidi ya Isoso Sekondari.
Aidha kwa upande wa mashindano ya kukimbiza kuku kwa wazee, washindi ni Bi. Monica Charles na Bw.Patric Zengo na kisha wakatunukiwa kuondoka nazo.
Hata hivyo akizungumza wakati alipokuwa akimkaribisha Msimamizi wa sherehe za muungano Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe. Joel Ndettoson amezipongeza timu zote zilizoshiriki mashindano ya mpira wa pete na miguu na ameendelea kutoa wito kwa wananchi wote kushiriki mkesha wa kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano kiwilaya yatakayofanyika katika viwanja vya Shirecu April 25,2024.
Kwa upande wake Msimamizi mkuu wa sherehe za Muungano na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika mkesha utakaonza saa 1jion hadi asubuhi huku wafanyabiashara na wajasiliamali wakikaribishwa na bidhaa zao kwa lengo la kufanya biashara.
"Hongereni kwa uzalendo wenu mkubwa mliouonesha na kuheshimu muungano wetu, kiukweli miaka 60 bado tumelelewa kwenye amani,utulivu na upendo hivyo tuendelee kutembea katika hayo kama ilivyo desturi yetu watanzania kesho tutakuwa sehemu moja tu Shirecu tutakabidhi zawadi kwa washindi na pia tutapata burudani mbalimbali usalama upo wa kutosha" ,ameongeza Mkude.
Msimamizi mkuu wa sherehe za muungano na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Joseph Mkude akizungumza wakati akihitimisha kilele cha bonanza la michezo April 24,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe wilayani humo kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Katikati ni mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu Bw.Masesa Kuzenza,kushoto Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson na kulia ni Msimamizi wa sherehe za Muungano na mkuu wa Wilaya ya Kishapu Aprili 24,2024 kwenye kilele cha bonanza la michezo kuelekea miaka 60 ya muungano
Katikati ni muamuzi wa mchezo wa mpira wa pete mwl. Baraka Mwakilili,kushoto Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson na kulia ni Msimamizi wa sherehe za Muungano na mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude Aprili 24,2024 kwenye kilele cha bonanza la michezo kwelekea miaka 60 ya muungano
Diwani wa kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettoson akizungumza kwenye kilele cha bonanza la michezo April 24,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe wilayani humo kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Msimamizi mkuu wa sherehe za muungano Wilaya ya Kishapu kwenye kilele cha bonanza la michezo aliyoifunga Aprili 24,2024 Mhe. Joseph Mkude akipiga danadana kwenye viwanja vya michezo vya shule ya msingi Buduhe wilayani humo mkoani Shinyanga.
Picha ya pamoja ya wachezaji wa Kishapu Veteran wanawake na msimamizi mkuu wa sherehe za muungano Mhe. Joseph Mkude na Diwani ya kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson kabla ya mechi wakiwachapa bao 8-5 Isoso Sekondari kwenye kilele cha bonanza la michezo lililohitimishwa April 24,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano
Picha ya pamoja ya wachezaji wa Isoso Sekondari na msimamizi mkuu wa sherehe za muungano Mhe.Joseph Mkude na Diwani ya kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson kabla ya mechi waliopigwa bao 8-5 dhidi ya Kishapu Veteran wanawakeApril 24,2024 kwenye kilele cha bonanza la kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano
Picha ya pamoja ya wachezaji wa Kishapu veteran na msimamizi mkuu wa sherehe za muungano Mhe.Joseph Mkude na Diwani ya kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson kabla ya mechi waliochapwa 0-1 dhidi ya GhazzaApril 24,2024 kwenye kilele cha bonanza la kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano
Mshindi aliyeshiriki mashindano ya kukimbiza kuku Bw.Patrick Zengo katika finali za bonanza april 24,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Bi. Monica Charles aliyeshiriki mashindano ya kukimbiza kuku kwenye mashindano ya kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano yaliyofanyika April 24,2024 kwenye viwanja vya shule ya Msingi Buduhe Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga
Msimamizi mkuu wa sherehe za muungano na mkuu wa wilaya ya Kishapu Mkaoani Shinyang Mhe.Joseph Mkude Kushoto (aliyevaa traksuti) na Diwani wa Kata ya Kishapu(kulia mwenye nguo nyeupe) Mhe.Joel Ndettoson wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Isoso Sekondari kwenye kilele cha bonanza la michezo April,24,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Buduhe wilayani humo.
Picha ya pamoja ya wachezaji wa Ghazza Fc na msimamizi mkuu wa sherehe za muungano Mhe.Joseph Mkude na Diwani ya kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson kabla ya mechi walioibuka kidedea kwa bao 1-0 dhidi ya Kishapu Veteran April 24,2024 kwenye kilele cha bonanza la kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano