Wizara ya Kilimo kupitia Bajeti yake ya mwaka 2023/2024 imenunua Vishkwambi 4446, kati ya hivyo vishkwambi 946 vimesambazwa na usambazaji unaendelea kwa ajili ya usajili wa wakulima, kukusanya taarifa, kuchukua alama ya nukta katika mashamba ya wakulima na utoaji huduma za ugani kwa njia ya kidijiti na kuwawezesha maafisa ugani katika ngazi ya kata kukusanya na kuingiza takwimu kwenye mfumo wa ARDS.
Aidha, katika kuhakikisha wakulima wanafanya kilimo chenye tija, Wizara ya Kilimo imeanzisha kituo cha huduma za ushauri kwa Wakulima (Call centers) na kununua vifaa vya huduma za ugani katika Halmashauri 166 nchini.
Social Plugin