MJUMBE wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT)Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa jumuiya hiyo Marima Ulega amekabidhi simu za mkononi tisa kwa ajili ya kufanikisha usajili wanachama kieletroniki ndani ya Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na wana UWT Mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kukabidhi simu hizo Mariam Ulega amesema kwa sasa wanaona na wanaendelea kujivunia matunda ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na hakika amekuwa mwananmke shupavu na mwenye mapenzi makubwa na wanawake wa Tanzania hasa UWT.
Amesema siku za hivi karibuni walipatiwa semina na viongozi wa UWT Taifa wakiongozwa na Mwnyekiti wao Mary Chatanda na katika semina hiyo walieleza masuala mbalimbali hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji na kubwa zaidi wamehimizwa kufanya kazi.
“Sisi wana UWT tufanye kazi na tupite kwa wananchi tukielezea mazuri yaliyofanywa na Rais.Hatuwezi kufanikiwa kama hatuna ongezeko la wana chama hivyo tunatakiwa tuwavute wanachama wapya , tusajili wanachama wapya kieletroniki na hiyo itatusaidia.
“Tunafahamu wapo akina mama wenzetu wanaojishughulisha na mama lishe, wajasiriamali na wapo waliopo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.Hivyo sisi kama jeshi la mama Samia tunatakiwa tutoke kuhakikisha tunavuna wanachama wengi,”amesema.
Amefafanua kuna mtandao wa UWT ambao umeanzishwa unaosajili wanachama keletroniki na Mkoa wa Pwani kuna wilaya moja ndjo inaonekana inasajili wanachama.Hata hivyo kunachangamoto ya vitendea kazi.
“Hivyo nimeamua na nimedhamiria kwa dhati kusaidia jumuiya hii, hivyo nimeamua kuleta simu kwa ajili ya kufankisha usajili wa kieletroniki katika mkoa wetu ili taarifa za usajili zinapotunwa na mkoa wetu uwepo .
“Makatibu wa UWT naaawamini hivyo tuhakikishe tunahamasisha wanachama wapya kwa kuwasijili sambamba na kuwaelezea UWT ni nini na inafanya kazi zipi na iwapo watajiunga nayo watapata faida zipi.
“Mwenyekiti wetu wa UWT Taifa tunamuona anahimiza usajili, tukiwa na wanachama wengi tutasonga mbele hivyo simu janja ninazokabidhi zinakwenda kurahisisha shughuli za usajili.”
Mariam Ulega amesema anatambua mkoa wa Pwani una wilaya nane lakini amegawa simu tisa kwani moja itakuwa simu ya mkoa ambayo itatumika kwa shughuli za usajili wa wanachama kama ambavyo itakuwa ikifanyika wilayani.“Hivyo twendeni tukaongeze wanachama kwa kasi ya 4G.”
Social Plugin