Na Mwandishi Wetu,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Pwani pamoja na wadau kutoka Mashirika mbalimbali wamefanya tathmini ya athari na uharibifu kwa waathirika wa mafuriko katika kata mbalimbali Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani ili kupata taarifa kamili zitakazoisaidia Serikali katika kuchukua hatua za muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kwa waathirika wa mafuriko yalitokea Wilayani humo.
Timu hiyo imetembelea leo (Aprili 17, 2024) katika kata ya Mkongo pamoja na Kata ya Ngorongo Wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Social Plugin