Wabunge wameunga mkono mpango wa kupiga marufuku mtu yeyote aliyezaliwa baada ya 2009 kununua sigara, na kuhakikisha kuwa itakuwa sheria.
Hatua hizo, zilizopigiwa upatu na Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, zilinusurika licha ya upinzani kutoka kwa viongozi kadhaa wakuu wa Tory - ikiwa ni pamoja na mawaziri wawili wa zamani.
Waziri wa afya Victoria Atkins aliwaambia wabunge kuwa "Hakuna uhuru katika uraibu" wakati akitetea mipango hiyo.
Mswada wa Tumbaku ulipitishwa kwa kura 383 dhidi ya 67. Ikiwa utakuwa sheria, sheria za uvutaji sigara za Uingereza zitakuwa kati ya kali zaidi ulimwenguni.
Mtazamo wa Uingereza unadhaniwa kuwa uliongozwa na sheria kama hiyo nchini New Zealand, ambayo baadaye ilifutwa baada ya mabadiliko katika serikali.
Akizungumza katika Baraza la Commons, Bi Atkins alisema mpango huo utaunda "kizazi huru cha moshi".
Hata hivyo, wabunge kadhaa wa Tory, akiwemo waziri mkuu wa zamani Liz Truss, walipiga kura dhidi ya muswada huo, wakisema utapunguza uhuru wa kibinafsi.
Social Plugin