Kampuni ya TIGO Tanzania imekabidhi zawadi ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa shindano la 'Soka la AFRIKA limeitika' kupitia kampeni ya Afcon 2023 iliyoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Bw. Raphael Songelaeli mkazi wa Shinyanga ameibuka mshindi na kujinyakulia kitita hicho cha fedha.
Zawadi hiyo imekabidhiwa leo April 25,2024 nyumbani kwa mshindi huyo mtaa wa viwanja vya Mwadui ndani ya manispaa ya Shinyanga.
Meneja wa Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga Sadock Mahundo amesema kampuni ya Tigo imeendelea kuendesha promosheni mbalimbali kwa wateja wake na kuendelea kutoa zawadi kwa washiriki wanaoibuka washindi kwa kuwafata hadi nyumbani ili kuongeza hamasa kwa wateja wake na kuboresha promosheni hiyo .
Meneja wa Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga Sadock Mahundo
"Kampeni hii ya 'Soka la AFRIKA limeitika' leo ilikuwa ni awamu ya kwanza ya promosheni hii ambayo ilikuwa inaenda sambamba na michuano ya Afcon 2023 iliyokuwa ikiendelea, nitumie fursa hii kuwaambia wateja wetu kwamba promosheni bado inaendelea na kwasasa imeboreshwa zaidi ambapo tutakuwa tunapata washindi wa kila siku ambaye atakuwa anajipatia shilingi Laki moja, tutakuwa tunafanya droo ya mshindi wa wiki ambaye atakuwa anajishindia shilingi la tano na kila mwezi mshindi atakuwa anajishindia shilingi Milioni moja", amesema Mahundo.
"Kushiriki ni rahisi utaingia kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi utaandika neno 'SOKA' na kisha kutuma kwenda namba 15670 na kujibu maswali mbalimbali na hatimae kuibuka mshindi, kwa tukio hili lililofanyika leo ni ushuhuda kuwa hakuna utapeli wa aina yoyote, katika promosheni zote kutoka kamuni ya TIGO zinaendeshwa kwa kuzingatia vigezo na masharti na ni rahisi kwa yeyote kuweza kushiriki", ameongeza Mahundo.
Akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea zawadi hiyo Bw. Raphael Songelaeli ameishukuru kamuni ya TIGO kwa kuendesha mashindano hayo na kiwasihi watu wengine kujiunga na mtandao wa TIGO ili waweze kushiriki na hatimae kuibuka washindi.
Mshindi wa shindano la 'Soka la AFRIKA limeitika' Raphael Songelaeli
"Mashindano ya Afcon 2023 yalipoanza nilianza kufatilia ambapo muda mwingi nilikuwa nautumia kucheza mara kwa mara na kuendelea kujikusanyia point hadi leo kuibuka mshindi wa mashindano haya ya 'Soka la AFRIKA limeitika' kwa kweli nawashukuru sana, fedha hizi nilizopata zitakwenda kunisaidia mimi na familia yangu, niwahamasishe na watu wengine kushirika mashindano mbalimbali yanayoendeshwa na mtandao wa TIGO ili na wao waweze kushinda", amesema Raphael Songelaeli.
Meneja wa Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga Sadock Mahundo akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mshindi wa shindano la 'Soka la AFRIKA limeitika' Raphael Songelaeli akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi.
Wafanyakazi wa Kamuni ya TIGO tawi la Shinyanga katika picha ya pamoja wakati wa kukabidhi hundi kwa mshindi.
Baadhi ya watu waliojitokeza katika hafla fui ya utoaji wa zawadi kwa mshindi wa Soka la AFRIKA limeitika.
Wasanii wa kundi la Kambi ya Nyani wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mwadui Manispaa ya Shinyanga Nuru Juma akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Meneja masoko wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Ziwa Musa Mwakapala akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa mshindi.
Social Plugin