Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO AKABIDHI MITUNGI YA GESI YA ORYX 1500 KWA WANANCHI ,WAJASIRIAMALI ARUSHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 

***************

 Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne barani Afrika wanapoteza maisha kila mwaka kwasababu ya kutumia nishati chafu ikiwemo ya kuni na mkaa.

Hivyo amesema ajenda ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuanzisha kampeni ya kuhamasisha nishati safi Afrika inapaswa kuungwa mkono na watu wote  huku akitumia nafasi hiyo kueleza matumizi ya kuni na mkaa nchini yanasababisha hekta 46242 kupotea kila mwaka kwasababu ya kuni na mkaa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali Dk.Jafo amesema hatua hiyo inakwenda kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa na dhamira njema na ndio maana amekuja na kampeni ya nishati safi ya kupikia.Haya ni mapenzi yake na kwasababu tunafahamu nishati chafu inamadhara makubwa katika mazingira.

“Kwanza watu wanalazimika kutegemea kuni na mkaa kwa hiyo kuna uharibifu wa mazingira.Takwimu zinaonesha kila mwaka hekta 46242 zinapotea kwasababu ya kuni na mkaa,”amesema Dk.Jafo.

Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa kina mama na wasichana kwa asilimia kubwa wanatumia wastani wa saa 20 kwa wiki kwa ajili ya kutafuta kuni na mkaa au wakati mwingine ni kinyesi cha wanyama.

“Leo hii ukiona nchi imejipanga katika nishati safi ya kupia ni jambo la msingi lenye kutia matumani.Watafiti  wanatuambia kitendo cha kutumia nishati safi ya kupikia kwa akina mama wajazito kunasaidia kurekebisha presha ya mama mjazito,”amesema.

Ameongeza pia nishati safi inasaidia mama mjazito kupata mtoto mwenye uzito unaokubalika anapozaliwa , hivyo kuna faida nyingi  kutumia nishati safi ya kupikia.

“Nina fahamu mpaka leo hii Oryx wameshatoa mitungi ya gesi 32,000 kwa ajili ya jamii na wameshatumia Sh.bilioni 2.7 lakini bado wameendelea kuendelea na kampeni hiyo kwa kutoa mitungi kwa jamii.

Ameongeza kuwa Oryx wamekuwa mfano mzuri kuifikia jamii  huku akifafanua tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa taasisi zinazoanzia watu 100 kufunga mfumo wa kutumia nishati safi ya kupikia na tayari taasisia na mashirika ya umma yameanza kutumia nishati hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia kuhamasisha nishati safi ya kupikia wameona ni vema kuendelea kuyagusa makundi mbalimbali katika jimbo hilo.

Amesema kuwa kabla ya kugawa mitungi hiyo 1,500 ya Oryx kwa wana Arusha Mjini, tayari ameshagawa pia mitungi 1400 kwa wajasiriamali huku akisisitiza wataendelea na kuyafikia makundi yote yakiwemo ya watoto wanaolelewa vituo vya ya watoto yatima.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman amempongeza Gambo kwa kuona umuhimu wa kuligusa kundi hilo kwa kuhakikisha linatumia nishati safi ya kupikia katika shughuli zao.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea madhara yanayotokana na kutumia kuni na mkaa ambapo amesema nchini  Tanzania, wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na kuni. Kupika na gesi ya Oryx itatatua jambo hili.

Aidha amesema kupika kwa kutumia gesi ya Oryx huzuia ukataji miti, kwa hiyo husaidia kulinda mazingira huku akieleza pia  kutumia gesi ya Oryx huzuia wanawake kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa msituni.

"Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx ni kupika kwa haraka na kwa ufanisi zaidi; kwa hiyo, wanawake wataanda chakula kwa wakati na wanaume hawatalalamika juu ya kuchelewa kwa chakula kinachosababisha mizogo.

"Kwa hivyo, Oryx Gas Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza maono ya Rais kuhusu upatikanaji wa nishati.Namshukuru Mbunge wa Arusha Mjini Gambo na serikali ya Tanzania  kwa kutuunga mkono katika mipango yetu ya nishati safi kwa kuhakikisha matumizi ya gesi ya Oryx hapa Arusha na Tanzania kwa ujumla". Ameeleza Araman

kwa upande mwingine wajasiriamali wameeleza kuwa hatua hiyo ya kupewa mitungi ya gesi inakwenda kuwaondolea adha waliyokuwa wakiipata kwa muda mrefu.

Wajasiriamali Asha Mtumwa na Karim Abdallah wamesisitiza kuwa ni jambo la kupongeza kuona kampuni ya Oryx inawakabidhi mitungi hiyo kwani inaenda kuondoa athari ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa matumizi ya kuni na mkaa ambapo inaathari kuanzia kwenye afya pamoja na mazingira.

Wamesema pia mitungi waliyokabidhiwa inakwenda kuwarahisishia shughuli zao kwa urahisi kutokana gharama nafuu ya gesi kuliko matumzi ya mkaa ambayo ni gharama na si rahisi kurahisisha kupikia.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akiwasikiliza mama lishe na baba lishe kwenye hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Baadhi ya watumishi wa Kampuni ya gesi ya Oryx wakiwa katika hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Oryx, Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Oryx wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha  
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemeni Jafo (katikati), Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ( wa kwanza kulia),Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Haji Ussi (GAVU) (wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Benoite Araman akiwa na watumishi wa Kampuni ya gesi ya Oryx wakiwa kwenye picha ya pamoja na mama lishe na baba lishe wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali leo Aprili 27,2024 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com