Ushauri huu umetolewa leo katika Tamasha la afya day lililoandaliwa na Taasisi ya Teknolojia Dar ES Salaam DIT kampasi ya Mwanza na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali waliojitokeza kushiriki na kupima afya zao.
Mganga mkuu wa Jiji la Mwanza Dr Sebastian Pima akimwakilisha Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amewaomba wananchi kuzingatia suala la afya kwa kufanya mazoezi pamoja na kula mlo kamili.
Mwakilisha wa mkurugenzi wa DIT , William Lohay amesema Tamasha la afya day ni utekelezaji wa mwongozo wa Serikali wa kuhakikisha afya za wafanyakazi zinakuwa imara.
Wataalam wa magonjwa ya ndani kutoka Hospital ya rufaa ya kanda Bugando wametoa huduma mbalimbali ikiwemo vipimo na ushauri wa namna ya ulaji Bora na kuzingatia mazoezi ili kujiepusha na maradhi na gharama ambazo zinaweza kujitokeza.
Baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu wameishukuru Taasisi ya DIT kampasi ya Mwanza kuwasogezea huduma za vipimo bure.
Awali Tamasha hilo lilianza kwa matembezi ya kilomita 6 yakijumuisha wafanyakazi na wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali na Shule za sekondari zilizopo mkoani Mwanza.