SAVANNAH PLAINS YATIKISA TENA KIMATAIFA, YARUDI NA USHINDI MASHINDANO YA DUNIA UBINGWA WA 'DEBATE'


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwenye Mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza na safari hii tena imerudi na ushindi na kutunukiwa tuzo, kombe na medali kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’.

Katika Mashindano hayo yaliyofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kuanzia Mei 9,2024 hadi Mei 12,2024 yakishirikisha nchi mbalimbali, Shule ya Sekondari Savannah Plains imepata ushindi wa Taasisi ya pili bora (The second best Institution), Washindi wa robo fainali (Quarter finalists), mzungumzaji bora wa Mdahalo kutoka Tanzania (The best debater from Tanzania) Hawarose Hassan Uledi, Mzungumzaji bora wa Nane (The eight best speaker)Allan Raymond Kabaya na imepata medali na tuzo ya washiriki bora wa mashindano.
Mratibu wa Somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi aliyeambatana na timu ya ushindi ya wanafunzi 25 wamepata ushindi katika mashindano hayo ya kidunia na kuendelea kuipa heshima na kuitangaza nchi ya Tanzania kimataifa.

“Tumerudi kutoka kwenye mashindano ya kidunia yaliyokuwa yanafanyika Kenya. Tunayo makombe matatu la kwanza tumekuwa washindi wa pili ngazi ya taasisi bora kwenye shule zote zilizoshiriki, tumepata washindi wawili waliofika ngazi ya robo fainali na tuzo ya wanafunzi waliofanya vizuri.

“Lengo la mashindano hayo ni kuwawezesha wanafunzi kujiamiani, kujieleza vizuri na kujifunza tamaduni mbalimbali za watu wanaokutana nao kutoka nchi mbalimbali. Wanafunzi wetu wamenufaika vitu vingi kwenye mashindano haya ikiwemo kujiamini ya kujieleza, kukutana na watu mbalimbali dunian, yanajenga watoto, tumetangaza nchi ya Tanzania”,amesema Kinyunyi.

Nao wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mashindano hayo ya African Debate Academy akiwemo Hawarose Hassan Uledi na Allan Raymond Kabaya wamesema mashindano hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwa shule, mkoa na taifa kwa ujumla kwani wameweza kushinda na kuitangaza nchi ya Tanzania ngazi za kimataifa.
Hawarose Hassan Uledi na Allan Raymond Kabaya (kulia).

“Nimeshinda sehemu ya kwanza Best All Debators from Tanzania yalikuwa mashindano mazito lakini tumejitahidi kufanya vizuri kama tulivyokuwa tumeahidi. Mashindano yametusaidia kutujengea uwezo wa kujiamini, kupata marafiki na kujifunza mambo mapya”,amesema Hawarose.

“Mambo yalienda vizuri sana, tumekutana na washiriki kutoka nchi mbalimbali. Kwa kizazi hiki mashindano haya yanatusaidia kujiamini na kutengeneza viongozi wa baadae ambao watakuwa na uwezo wa kutoa hotuba nzuri”,ameongeza Kabaya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya amesema ushindi huo unatokana na mazoezi ya kutosha yanayotolewa kwenye Idara ya Kiingereza na ushirikiano mkubwa unaotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nina furaha kubwa sana kuwapokea wanafunzi wangu ambao tuliwatuma kama Timu ya ushindi kwenda Nairobi Kenya kushiriki kwenye mashindano haya kwa kweli ushindi huu umeanzia mbali, tulianzia jijini Dar es salaam kwenye mashindano ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere ambapo tuliibuka washinda tukapata pointi za kwenda Afrika Kusini kushiriki ambapo tuliibuka washindi tukapata pointi za kutuwezesha kwenda kushiriki mashindano haya ya kidunia”,amesema Ludomya.

“Tumepiga kitaifa, tumepiga ki Afrika na sasa tumepiga Kidunia, siri yetu kubwa ni maandalizi mazuri ya watoto, wameandaliwa vizuri kupitia Idara ya Kiingereza hivyo kuweza kushiriki mashindano yoyote yale",amesema.
“Vijana wetu hawa waliorudi leo wamerudi na ushindi mkubwa kwa mara nyingine tena,wamerudi na makombe, wamerudi na ngao pamoja na medali, huu ni ushindi mkubwa kwa kweli tunaishukuru serikali ya Muungano wa Tanzania chini Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa na ushirikiano mzuri na nchi za mataifa mbalimbali kwa kupitia balozi mbalimbali tunajivunia, vijana hawa waliorudi na ushindi tunawategemea kuja kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali”,ameongeza Ludomya.


Amefafanua kuwa mashindano hayo yanamjenga mtoto kuwa na uwezo wa kujiamini na kuzungumza mbele ya hadhara hivyo kuiomba serikali iendeleze ushikiriano na nchi za Afrika Mashariki, Afrika na kimataifa ili kuwezesha Watanzania kushiriki mambo mbalimbali na nchi zingine.


“Vijana hawa ni wa Kitanzania, kote walikoenda wamejitambulisha kuwa ni Watanzania na wametangaza mambo mazuri yaliyopo Tanzania ikiwemo kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutangaza Utalii wa Tanzania”,amesema.

Shule ya Sekondari Savannah Plains ni miongoni wa shule zinazofanya vizuri. Shule hii ya bweni ipo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga mkabala na barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza.


Michepuo inayotolewa Savannah Plains High School ni PCM,PCB, PGM, HGE, EGM, HGL,HGK, HKL na ECA.

Kwa Mawasiliano zaidi +255 742 555 550 / 0743919187/0742919198
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga nchini Tanzania wakirejea kwa furaha shuleni wakiwa tuzo, kombe na medali za ushindi baada ya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’ yaliyofanyika nchini Kenya.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga nchini Tanzania wakirejea kwa furaha shuleni wakiwa tuzo, kombe na medali za ushindi baada ya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’ yaliyofanyika nchini Kenya.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga nchini Tanzania wakirejea kwa furaha shuleni wakimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya tuzo, kombe na medali za ushindi baada ya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’ yaliyofanyika nchini Kenya.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya akizungumza baada ya kuwapokea wanafunzi walioshiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’ yaliyofanyika nchini Kenya.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya (kulia) akipokea tuzo walizopewa wanafunzi wake walioshinda Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’. 
Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya (kulia) akipokea tuzo walizopewa wanafunzi wake walioshinda Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’. 
Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya akifurahia tuzo walizopewa wanafunzi wake walioshinda Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’. 
Zawadi zilizotolewa kwa shule ya Sekondari Savannah  baada ya kuibuka washindi kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’. 
Zawadi zilizotolewa kwa shule ya Sekondari Savannah  baada ya kuibuka washindi kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’. 
Mratibu wa Somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi  akielezea namna walivyoshiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’. 
Mratibu wa Somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi  akielezea namna walivyoshiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’.
Mwanafunzi mshindi Hawarose Hassan Uledi akielezea namna walivyoshiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mijadala na Kuongea kwenye hadhara Afrika Mashariki ‘The East African World debate Championship’.
Mwanafunzi mshindi Hawarose Hassan Uledi na Allan Raymond Kabaya 
Wanafunzi washindi Hawarose Hassan Uledi na Allan Raymond Kabaya 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post