MBUNGE wa Jimbo la Babati Mjini, Mhe. Pauline Philip Gekul ameibua shangwe, nderemo na vifijo bungeni Dodoma, baada ya kusimama na kugusia kidogo juu ya sakata la kesi yake.
Akichangia hoja katika makadirio ya mapato na matumizi, katika bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mbunge huyo mpole na mtumishi wa Mungu, ameeleza namna ambavyo 'alikinywea kikombe' katika wakati huo mgumu, na kwamba haikuwa rahisi.
"Namshukuru Mungu kwa namna ambavyo amekuwa akitubariki sote, Kila moja wetu kwa namna yake, hata pale tunapopitia magumu, yeye hutusaidia kwa namna ya kipekee," alisema na kuongeza;
"Hata mimi, katika kipindi kigumu nilichopitia, haikuwa rahisi kwamba leo nimeweza kusimama hapa, lakini kwa maombi ya Watanzani na kudra zake Mungu, leo nasimama kwa ujasiri kuendelea na majukumu yangu ya kibunge.
"Nimevipisha vyombo vya Sheria kuendelea na kazi yake, lakini ukweli utabainika, tujijengee Utamaduni wa kuwaombea viongozi wetu wa kitaifa.
"Pia nimshukuru sana Rais, Dkt. Samia kwa namna ambavyo ameniamini mimi binti yake, amenitoa mbali, ni mama msikivu, mwenye huruma na mzalendo wa kweli, Mungu akubariki Mhe. Rais na sisi wana Babati hatuna deni na wewe," amesema Mhe. Gekul kwa sauti ya ujasiri na busara thabiti.
Social Plugin