Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA, EWURA WAJIONEA MAAJABU YA MRADI MKUBWA KITUO CHA UZALISHAJI MAJI YA ZIWA VICTORIA KASHWASA - IHELELE

Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakitembelea Kituo cha uzalishaji ya Ziwa Victoria Kilichopo Ihelele wilayani Misungwi Mkoani Mwanza - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Na Marco Maduhu,MISUNGWI

WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi wametembelea Kituo cha uzalishaji ya Ziwa Victoria Kilichopo Ihelele wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, maji ambayo huzalishwa kupitia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (KASHWASA).

Ziara hiyo imefanyika leo Mei 3,2024 ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga juu ya kufahamu majukumu ya EWURA kwa kutembelea kituo hicho ili kujifunza kwa vitendo,ambapo leo pia ni siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Kituo hicho za uzalishaji Maji ya Ziwa Victoria Ihelele, licha ya kusambaza Maji katika Mkoa wa Shinyanga na Mikoa jirani kwa sasa maji yanafika hadi Shelui mkoani Singida.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher akizungumza kwenye ziara hiyo, amesema ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo ili waandishi wa habari wafahamu vizuri majukumu ya EWURA na kuona namna ya uzalishaji wa Maji kutoka Ziwa Victoria.

"Ziara hii ni sehemu ya mendelezo wa mafunzo yetu ya EWURA kwa Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga,ambayo tulianza jana na leo tumetembelea mradi huu wa uzalishaji Maji ya Ziwa Victoria tuna imani wamejifunza mengi juu ya uzalishaji huu na gharama zake",amesema Mhandisi Christopher.

Kaimu Mkurugenzi wa KASHWASA John Zengo ambaye ni Meneja huduma kwa wateja, amesema Mradi huo wa uzalishaji Maji ya Ziwa Victoria ulianza kujengwa mwaka 2002-2003 chini ya Rais Hayati BenjaminiMkapa na ulikamilika mwaka 2008 na kuanza kutoa huduma ya Maji rasmi mwaka 2009 katika Miji ya Shinyanga na Kahama.

Amesema uwezo wa Mradi huo ni kuzalisha Maji Lita Milioni 80 kwa Siku, lakini kwa sasa wanazalisha Lita Milioni 67 kutokana na uchache wa wateja, ambapo kwa sasa wanahudumia Mikoa Sita hadi Shelui mkoani Singida.

"Mradi huu wa kuzalisha Maji ya Ziwa Victoria ulianza kutokana na Miji ya Shinyanga na Kahama kuwa na Shida kubwa ya Maji,"amesema Zengo.

Amesema wao KASHWASA wamekuwa wakizalisha Maji ya Ziwa Victoria kutoka Ihelele, na kuziuzia Mamlaka nyingine za Maji, ambazo nazo zinawauzia wananchi na kupata huduma hiyo ya Maji Safi na Salama.

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Kaimu Mkurugenzi wa KASHWASA John Zengo ambaye ni Meneja huduma kwa wateja
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakisikiliza maelezo namna maji yanavyozalishwa kutoka ndani ya Ziwa Victoria.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakisikiliza maelezo namna maji yanavyozalishwa kutoka ndani ya Ziwa Victoria.
 
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakisikiliza maelezo namna maji yanavyozalishwa na kutibiwa kutoka ndani ya Ziwa Victoria.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakisikiliza maelezo namna maji yanavyozalishwa na kutibiwa kutoka ndani ya Ziwa Victoria.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mamlaka ya kudhibiti huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi wakiangalia namna maji yanavyotibiwa ili yawe salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com