MAJI, UMEME NA BARABARA VYAWACHARUA MADIWANI KISHAPU


Kaimu Meneja Tanesco Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhandisi Khamis Mbembe  akielezea mkakati wa miradi mbalimbali ya uunganishaji umeme kwa wananchi  wa Kishapu ifikapo 2025 vijiji vyote viwe vimepata huduma hiyo leo alipokuwa kwenye baraza la madiwani la uwasilishwaji taarifa za Kata  leo Mei,8,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo

Na Sumai Salum - Kishapu

Madiwani wa Jimbo la Kishapu wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wamesikitishwa na kasi  ya usambazaji  umeme,maji na ukarabati wa miundombinu ya barabara suala linalopelekea wao kupokea maswali mengi kutoka kwa wananchi wanaowawakilisha.

Wakihoji maswali kuhusiana na kero hizo leo Mei,8,2024 katika baraza la Madiwani la uwasilishwaji taarifa za Kata lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wawakilishi wa kata za Kishapu, Shagihilu,Mwakipoya,Somagedi,Itilima,Ndololeji pamoja na Ngofila wamesema miradi ya umeme inasuasua katika uwekaji nguzo na hata kucheleweshwa usambazaji kwa wateja ambao ni wananchi.

Diwani wa Kata ya Itilima Mhe. Lameck Subata amesema kuwa miongoni mwa vipaumbele ambavyo Tanesco wanatakiwa wahakikishe wanasogeza huduma kwa haraka ni pamoja na taasisi zote za serikali ikiwemo Zahanati na mashuleni.

Akijibu  maswali ya madiwani   Kaimu meneja Tanesco Wilaya Mhandisi Khamis Mbembe amethibitisha kucheleweshwa kwa ukamilishwaji wa miradi hiyo hivyo watahakikisha wanasimamia vyema mkandarasi ambaye wanae (Suma JKT) ahakikishe anaongeza kasi ya utekelezaji miradi hiyo huku akiwahakikishia wateja wa majumbani kwa atakehitaji kusogezewa huduma ya umeme ndani ya siku tatu(3) anapewa namba ya malipo kisha kuunganishiwa huduma hiyo muhimu.

Aidha akijibu maswali ya  madiwani waliohoji kuhusu uunganishwaji wa maji kutoka Ziwa Victoria katika maeneo ya Seseko,Mpumbula,Bubiki,Bunambiyu,Mwamalasa pamoja na maeneo mengine ya Wilaya Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima amesema Mamlaka  inaendelea na utatuzi wa changamoto hizo huku baadhi ya maeneo hatua za awali tayari zimekamilishwa na maeneo mengine wanaendelea na taratibu zingine kwa mujibu wa sheria kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi.

"Waheshimiwa ni kweli huduma hii ni muhimu na Ruwasa inahakikisha inafanya bidii kwa kuandikia maandiko kwenye miradi inayohitaji fedha nyingi ukiwemo mradi wa Mwabusiga,na kwa Mwamalasa tayari hii leo tumempeleka Local fundi kwa ajili ya kuanza hatua za awali na vifaa vipo ofsini,kwa Masanga-Ndololeji tunasubiria maji yapungue kwenye chanzo cha mto kisha mwezi wa nane tunaanza kushughulikia na pia kwa kushirikiana na Ijumaa hii tarehe 10,2024 kwa kushirikiana na KASHWASA tunaunganisha katika kijiji cha Seseko,Mpumbura", amesema Mhandisi Kamazima.

Kaimu Meneja TARURA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Hussein Shaweji akijibu maswali ya madiwani kuhusiana na ubovu wa miundombinu ya barabara nyingi za Wilaya kutopitika na zingine kupitika kwa shida huku zikitegemewa kuwa sababu ya kukuza mapato ya Halmashauri amesema tayari wameshafanya upembuzi yakinifu tangia Novemba hadi Februali mwaka huu na baadhi ya barabara zinaendelea na ukarabati.
Kushoto ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Willium Jijimya na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Kishapu Dr.Sabinus Chaula wakiwa kweye kikao cha baraza la madiwani la uwasilishwaji wa taarifa za Kata leo Mei,8,2024 katika ukumbi wa Halmashaur hiyo.
Diwani wa kata ya Bubiki Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. James Kasomi akihoji Ruwasa kuhusu ukosekanaji wa huduma ya maji ya Ziwa Victoria katika kata yake kwenye baraza la madiwani la upokeaji taarifa za Kata lililofanyika leo Mei 8,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Meneja Ruwasa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Dickson Kamazima akijibu maswali kwenye baraza la madiwani la kupokea taarifa za Kata leo Mei,8,2024 lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kuhusiana na upungufu na ukosefu wa huduma ya maji ya Ziwa Victoria kwa baadhi ya vijiji na kata za Wilaya hiyo
Baadhi ya Madiwani Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani la kuwasilishwa taarifa za Kata zao leo Mei,8,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mhe.Abdul Nkolomole Diwani wa Kata ya Songwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga akizungumza leo mei 8,2024 kwenye baraza la madiwani la upokeaji taarifa za Kata lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashuri hiyo
Kaimu Katibu tawala Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Fadhiri Mvanga akiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani la uwasilishwaji taarifa za Kata lililofanyika leo Mei,8,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Diwani wa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Joel Ndettoson akifurahia hoja za baraza la madiwani la uwasilishwaji taarifa za Kata lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo leo Mei,8,2024.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post