Wakazi wa wilaya ya Mukono wameshangazwa baada ya mwanaume mmoja kudaiwa kuuawa akiwa usingizini na mkewe mwenye umri wa miaka 30.
Inadaiwa Ruth Musimenta amemchoma kisu shingoni James Nsubuga na kusababisha kifo chake.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Jumamosi, Mei 18,2024 katika makazi yao katika kijiji cha Katikamu.
Kama ilivyoripotiwa na Monitor, Fred Enanda, msemaji wa polisi, alifichua kuwa Musimenta alimfungia mumewe chumbani kwao kwa siku kadhaa na alipanga mpango wa kuutupa mwili wake.
“Nsubuga alichomwa kisu na mkewe shingoni akiwa usingizini hali iliyopelekea kifo chake. Mtuhumiwa aliuweka mwili huo chumbani kwa siku mbili hadi ulipotolewa na polisi.
Maafisa walipata kisu kinachohisiwa kutumika kwenye chumba cha kulala. Buti mbili za jeshi na bastola zilipatikana,” alisema.
Enanga pia alifichua kuwa Musimenta alikiri kosa la kumuua mumewe na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.
Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa mshukiwa na marehemu walikuwa na uhusiano wenye misukosuko, ambao hatimaye uliishia kwenye kisa hicho cha kutisha.
Social Plugin