Mamia ya watu wakiwemo Maaskofu, Mapadre, Watawa na waamini kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Jimbo la Shinyanga pamoja na viongozi wa vyama na Serikali, jana wamejitokeza kwa wingi kumsindikiza katika safari yake ya mwisho hapa duniani aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Ndala, Jimbo Katoliki Shinyanga Hayati Padre Emmanuel Makolo, ambaye amezikwa katika Makaburi ya Mapadre yaliyopo Kanisa kuu Ngokolo mjini Shinyanga.
Ibada ya Mazishi ilitanguliwa na Misa ya kumwombea Marehemu, ambayo iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Flavian Kassala, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC.
Akitoa mahubiri kupitia Misa hiyo ya Mazishi, Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, aliwasihi waamini kuendelea kumwombea Marehemu Padre Makolo, pamoja na kusimama imara kwenye imani yao hata pale wanapokutana na mahangaiko ya aina mbalimbali katika maisha yao.
Askofu Sangu alimwelezea Marehemu Padre Makolo kuwa alijitoa bila kujibakiza kupitia karama mbalimbali ambazo Mungu alimjalia katika utume wa Kanisa, huku watu mbalimbali waliopata fursa ya kutoa salamu zao za rambirambi, wakiwemo Maaskofu waliotoka nje ya Jimbo la Shinyanga, Mapadre na viongozi wa Serikali wakimwelezea marehemu kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika masuala ya kiroho na shughuli za maendeleo na kijamii, kupitia vipaji vingi ambavyo Mungu alimjalia.
Mazishi ya Hayati Padre Makolo yalihudhuriwa pia na Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande, wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali ambao ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Magile Anold Makombe ambaye alimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Paschal Patrobas Katambi, aliyewahi kuwa Mbunge wa viti maalu mkoa wa Shinyanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Azah Hilal pamoja na wajumbe wa Kamati ya Amani na Maridhiano ya Wilaya ya Shinyanga ambayo Hayati Padre Makolo alikuwa Mwenyekiti wake.
Padre Makolo alizaliwa mnamo Aprili 22 mwaka 1958, katika kijiji cha Mwamagembe Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Baada ya kumaliza elimu ya majiundo yake ya Kipadre, alipewa Daraja takatifu la Upadre mnamo Julai 2 mwaka 1987, katika Parokia ya Ndoleleji, ambapo baada ya kufanya utume wake katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Jimbo la Shinyanga ikiwemo katika chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino SAUT, mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Paroko wa kwanza wa Parokia ya Ndala mpaka alipofariki dunia.
Padre Makolo amefariki Dunia Aprili 25 mwaka 2024, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando Jijini Mwanza.
Mungu ailaze mahali pema Minguni roho ya Marehemu Padre Emmanuel Makolo…Amina
Mashemasi na Mapadre wakiwa kwenye maandamano kuingia Kanisa kuu la Ngokolo kwa ajili ya Misa ya Mazishi ya Marehemu Padre Emmanuel Makolo
Maaskofu wakiwa kwenye Maandamano kuingia Kanisani kwa ajili ya Misa ya kumwombea Marehemu, wa kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu na kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza Mhashamu Liberatus Sangu
Kiongozi wa Misa Askofu wa Jimbo Katoliki Geita na Makamu wa Rais wa Baraza la maaskofu Katoliki Tanzania TEC Mhashamu Flavian Kassala akiwa kwenye maandamano kuingia Kanisani.
Askofu Kasala akifukiza ubani Mwili wa Marehemu, mbele yake ni Shemasi Japhet Nyarobi wa Jimbo la Shinyanga ambaye kwa sasa anafanya utume katika Parokia ya Shinyanga mjini
Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bukundi Padre Emmanuel Gembuya akisomo Historia ya Marehemu
Askofu Kassala akiendelea na adhimisho la Misa
Wanakwaya
Shemasi Paschal Masunga wa Jimbo la Shinyanga anayefanya utume katika Parokia ya Mwanhuzi akisoma somo la Injili
Askofu Sangu akitoa mahubiri
Baadhi ya Mapadre wakifuatilia Mahubiri
Walelewa wa Shirika la Kijimbo katika Jimbo la Shinyanga la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma
Watawa
Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo la Shinyanga kulia akiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza Renatus Nkwande wa kushoto, pembeni ni Mashemasi
Mapadre na Mashemasi
Viongozi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama, katikati mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyaga Anamringi Macha wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo
Misa inaendelea
Bi. Suzana Mbuke Emmanuel ambaye ni Mama mzazi wa Mareheu Padre Makolo akikomunika
Askofu Mkuu Renatus Nkwande wa Jimbo kuu la Mwanza akitoa salamu za rambirambi
Askofu Flavian Kassala wa Jimbo la Geita akitoa salamu za rambirambi
Mwenyekiti wa umoja wa Mapadre wazalendo (UMAWATA) Jimbo Katoliki Shinyanga Padre Deusdedith Mhula akitoa salaam za rambirambi na neno la shukrani kwa aniaba ya Mapadre wa Jimbo la Shinyanga
Mwakilishi wa WATAWA akitoa salamu za rambirambi
Mwakilishi wa Kamati ya Amani na Maridhiano Wilaya ya Shinyanga ambayo Marehemu Padre Makolo alikuwa Mwenyekiti wake akitoa salam za rambi rambi kwa niaba ya Kamati nzima
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akitoa salamu za rambirambi
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Magile Anold Makombe ambaye alimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Paschal Patrobas Katambi akitoa salamu za rambirambi
Askofu Mkuu renatus Nkwande akiongoza sala ya Buriani
Maaskofu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu
Mapadre wakitoa heshima za mwisho
Viongozi wa Serikali wakitoa heshima za mwisho
Mwili wa Marehemu ukipelekwa kwenye Makaburi ya Mapadre nje ya Kanisa kwa ajili ya Mazishi, ndugu wa Marehemu wakiwa wamebeba Mashada ya maua
Askofu Sangu akiongoza Ibada ya mazishi
Askofu Sangu akibariki kaburi
Mapadre kwa kusaidiana na Mashemasi wakiweka kaburini Jeneza lenye Mwili wa marehemu Padre Emmanuel Makolo
Askofu Sangu akiandika ishara ya Msalaba kwenye Kaburi la Padre Makolo
Askofu Sangu akiweka Msalaba kwenye kaburi la Padre Makolo
Askofu Sangu akiweka shada la maua kwenye kaburi la Padre Makolo
Askofu Mkuu Renatus Nkwande na Askofu Flavian Kassala wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Padre Emmanuel Makolo
Mama mzazi wa Marehemu Padre Emmanuel Makolo Bi.Suzana Mbuke Emmanuel akiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wake.
Mapadre wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la Marehemu
Wawakilishi wa makundi mbalimbali wakiwemo Mashemasi, watawa na viongozi wa Serikali wakiweka shada la maua
Askofu Sangu akitoa baraka mara baada ya Ibada ya mazishi
CHANZO - RADIO FARAJA FM
Social Plugin