Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nguruwe Project kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Simon Mnkondya maarufu Mr Manguruwe amegawa bure tiketi 100 kwa Mashabiki wa Soka kwa ajili ya kushuhudia mchezo kati ya Simba SC na Dodoma Jiji utakaofanyika kesho Ijumaa Mei 17,2024 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mr Manguruwe ambaye ni shabiki kindakindaki wa Timu ya Simba SC amegawa tiketi hizo leo katika soko la Machinga Complex Dodoma.
"Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini kama ilivyo kwa Rais wa serikali ya Jamhuri ya mlmuungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akinunua magoli katika vilabu vya Simba SC na Yanga leo hii nimegawa tiketi 100 kwa mashabiki kuelekea mechi ya Dodoma Jiji dhidi ya Simba SC mchezo utakaopigwa katika uwanja vya Jamhuri Dodoma", amesema Tajiri huyo wa Nguruwe maarufu Mr Manguruwe.
Wasiliana na Mr Manguruwe kwa simu namba Namba +255763755755
Tazama Video HAPA
Soma pia
HABARI
BOSI WA KIJIJI CHA NGURUWE AAHIDI ZAWADI YA NGURUWE ALIYENONA KWA KILA GOLI LA SIMBA SC DHIDI YA IHEFU SC
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nguruwe Project kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ambaye ni shabiki kindakind…
MATUKIO
MCHEZAJI WA SIMBA SC 'CLATOUS CHAMA' APEWA ZAWADI YA NGURUWE MWENYE MIMBA
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nguruwe Project kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ambaye ni shabiki kindakinda…
Social Plugin